Ripoti ya hivi karibuni ya KM, kuhusu hali ya watoto kwenye mazingira ya mapigano yaliopamba katika JKK imethibitisha kuteremka idadi ya vitendo vilivyokiuka sana haki za watoto nchini. Ripoti ilbainisha kupatikana maendeleo machache kwenye zile juhudi za kuwapokonya watoto silaha na kuwajumuisha kimaisha kwenye jamii za kawaida. Juu ya hivyo, ripoti ilisisitiza, watoto bado wanaendelea kuwawa mwanzo kuathiriwa kwenye mgogoro wa katika Kivu Kaskazini na Kusini pamoja na Katanga Kaskazini. Kadhalika, ripoti iliendelea kusema, watoto wenye umri mdogo hulazimishwa kushiriki kwenye mapigano, na wakati huo huo wanaendelea kunajisiwa na makundi mbalimbali yenye silaha, vitendo ambavyo, ripoti ilisema, vinafanyika kwa wingi zaidi kwenye maeneo ya vurugu.