Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi tatu zakutikana kuvunja sheria ya Mkataba Dhidi ya Mabomu ya Kutega

Nchi tatu zakutikana kuvunja sheria ya Mkataba Dhidi ya Mabomu ya Kutega

Ripoti ya 2008 kuhusu namna Mataifa Wanachama yanavyotekeleza yale mapendekezo ya Mkataba wa Kupiga Marufuku Matumizi ya Mabomu Yaliotegwa Ardhini, iliowakilishwa rasmi hii leo katika UM, imebainisha nchi tatu wanachama zimeharamisha kanuni za Mkataba huo, kwa kushindwa kuangamiza silaha hizo kwa wakati; mataifa yenyewe ni Ugiriki, Uturuki na Belarus.