Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaribio la Mapinduzi Guinea-Bissau limelaaniwa na KM Ban

Jaribio la Mapinduzi Guinea-Bissau limelaaniwa na KM Ban

Kwenye risala iliotolewa, kwa kupitia msemaji wake, KM Ban Ki-moon ameshtumu vikali mashambulio ya Ijumapili dhidi ya makazi ya Raisi Bernardo Joao Vieira, yaliotukia Bissau, mji mkuu wa Guinea-Bissau yalioendelezwa na baadhi ya wanajeshi, wiki moja tu baada ya kufanyika uchaguzi wa bunge nchini humo.