Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya ushikamano na Wafalastina/BK kujadilia Falastina na Mashariki ya Kati

Siku ya ushikamano na Wafalastina/BK kujadilia Falastina na Mashariki ya Kati

Kwenye ukumbi wa Baraza la Udhamini asubuhi ya leo kumefanyika kikao maalumu, kilichodhaminiwa na Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Haki Zisofutika za Umma wa Falastina kuhishimu Siku ya Ushikamano na Umma wa Falastina kwa kulingana na azimio la Baraza Kuu la UM liliopitishwa mwezi Disemba 1977.

Vile vile alasiri Baraza Kuu la UM litakutana kuzingatia suala la Falastina, kwa kujadilia haki wanazonyimwa za kimsingi na vile vile kuzungumzia hali, kwa ujumla, katika eneo la Mashariki ya kati.