Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Ripoti ya hivi karibuni ya KM, kuhusu hali ya watoto kwenye mazingira ya mapigano yaliopamba katika JKK imethibitisha kuteremka idadi ya vitendo vilivyokiuka sana haki za watoto nchini. Ripoti ilbainisha kupatikana maendeleo machache kwenye zile juhudi za kuwapokonya watoto silaha na kuwajumuisha kimaisha kwenye jamii za kawaida. Juu ya hivyo, ripoti ilisisitiza, watoto bado wanaendelea kuwawa mwanzo kuathiriwa kwenye mgogoro wa katika Kivu Kaskazini na Kusini pamoja na Katanga Kaskazini. Kadhalika, ripoti iliendelea kusema, watoto wenye umri mdogo hulazimishwa kushiriki kwenye mapigano, na wakati huo huo wanaendelea kunajisiwa na makundi mbalimbali yenye silaha, vitendo ambavyo, ripoti ilisema, vinafanyika kwa wingi zaidi kwenye maeneo ya vurugu.

Kutokana na utulivu wastani huo Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeweza kupata upenu wa kugawa tani 100 za chakula katika sehemu ya Rutshuru, kwa wale raia wahaimaji wa ndani ya nchi. Katika kambi ya wahamiaji hao ya Kibati, Shirika la Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) nalo limeanza operesheni za kusajili watoto wa skuli waliokosa makazi kwa sababu ya mapigano; na imeanza kuwapatia vifaa vya masomo watoto karibu 1,000 itakayowawezseha kuhudhuria madarasa katika siku za karibuni.

Hii leo asubuhi KM alihudhuria kikao maalumu cha kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Umma wa Falastina. Alisema kwenye risala yake ana wasiwasi mkubwa kuhusu hali za raia ambao wamebanwa hivi sasa na vikwazo vilioekewa Tarafa ya Ghaza na Israel. KM alipendekeza vikwazo hivyo viondoshwe haraka, kitendo ambacho, alikumbusha, ndio kilichochea upungufu mkubwa wa vifaa vya kimsingi vinavyohitajika kukidhi mahitaji ya umma. KM aliongeza kusema kwamba Israel inawajibika kujizuia kutekeleza maamuzi ya upande mmoja, kuhusu mji wa Jerusalem, mathalan, maamuzi ya kufukuza watu makazi na kubomoa kihorera majumba yao, vitendo ambavyo, alisisitiza KM, hudhoofisha hali ya kuaminiana na hubadilisha hadhi halali iliokuwepo ya sheria. Wakati huo huo alisema anatambua mahitaji ya usalama ya wenye madaraka Israel.

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetangaza siku ya leo, kutokea Nairobi, ombi la kupendekeza ifadhiliwe dola milioni 400 kuzisaidia zile jamii muhitaji katika Kenya, hususan jamii ziliaoathirika na vurugu liliofumka nchini humo kufuatia kumalizika uchaguzi wa taifa katika mwisho wa mwaka uliopita. Kadhalika, kutokea Dakar, Senegal OCHA imeomba ipatiwe msaada wa dola milioni 360 kukabiliana na mzozo wa chakula kwa maeneo muhitaji ya Afrika Magharibi kwa mwaka 2009.