Uchambuzi wa Mratibu wa UM juu ya Udhibiti wa Homa ya Mafua Kimataifa

Uchambuzi wa Mratibu wa UM juu ya Udhibiti wa Homa ya Mafua Kimataifa

Karibuni, Dktr David Nabarro, Mratibu wa UM juu ya Udhibiti Bora wa Mripuko wa Maradhi ya Homa ya Flu Ulimwenguni alikutana na waandishi habari wa kimataifa waliopo katika Makao Makuu ya UM kuelezea maendeleo katika maandalizi ya kukabiliana na janga hili. Alitahadharisha ya kwamba wataalamu wa afya wanaashiria janga la maradhi ya homa ya mafua ya ndege huenda likaripuka ulimwenguni wakati wowote, kwa sababu ya mwelekeo wa kihistoria juu ya duru ya mifumko ya maradhi haya katika ulimwengu.

Alisema Mataifa Wanachama yote yanawajibika kuhakikisha, mara kwa mara, kama miradi walioitayarisha kukabiliana na janga la kufumka kwa maradhi ya homa ya mafua kitaifa inaridhisha.

Sikiliza taarifa kamili ya Dktr Nabarro kwenye idhaa ya mtandao.