Uhamisho wa mara kwa mara wadhuru afya ya watoto na wanawake, yahadharisha UNICEF

Uhamisho wa mara kwa mara wadhuru afya ya watoto na wanawake, yahadharisha UNICEF

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limeeleza ya kuwa uhamisho wa mara kwa mara unadhuru sana kihali na kiakili watoto na wanawake – hali ambayo mara nyingi huchochea hatari ya kufumka maradhi ya kipindupindu na shurua, pamoja na ongezeko la utapiamlo mbaya miongoni mwa watoto.