Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale (Taarifa za Kusoma)

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kwamba wiki iliopita watu 12,000 waliuhajiri mji wa Mogadishu, Usomali kwa sababu ya mapigano makali yaliozuka baina ya wapiganaji wafuasi wa makundi ya KiIslam, wenye kupinga serikali, dhidi ya na vikosi vya serikali vinavyoungwa mkono na majeshi ya Ethiopia yaliopo nchini. Nusu ya wahamiaji waliong’olewa makwao walipatiwa makazi ya muda karibu na mji, na nusu nyengine walikimbilia mji wa Afgooye ,uliopo kilomita 3o kusini-magharibi ya Mogadishu.

Mukhtasari wa siku ya pili ya majadiliano ya jumla katika Baraza Kuu

Waziri Mkuu wa Uchina Wen Jiabao aliwaambia wajumbe waliohudhuria kikao cha wawakilishi wote cha Baraza Kuu kwamba sera adhimu ya taifa lake ni kufuatilia njia ya amani kukuza maendeleo,wakati ikijenga nguvu za kijeshi kwa makusudio pekee ya kulinda na kuhami uhuru wake na umoja wa nchi. Alisema Uchina hauna dhamira yeyote ya “kumiliki dunia, si sasa wala si katika siku zijazo.” Alifahamisha kwamba nchi yake haitishii taifa lolote, na kusisitiza Uchina inajivunia pakubwa kwa mafanikio yake katika ustawi wa kiuchumi, kuendeleza haki ya jamii, upole wa raia zake na uadilifu wenye nguvu.~

Raisi wa Kenya asema taifa limepiga hatua muhimu baada ya vurugu

Majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote, yaliendelea mnamo alasiri ya siku ya mwanzo ya mahojiano ambapo Raisi Mwai Kibaki wa Jamhuri ya Kenya, alipohutubia mkutano, alisema nchi yake imepiga hatua muhimu kwenye maafikiano ya kurekibisha sheria, katiba na masuala mengine yanayaohitajika kutekelezwa ili kuepukana na na hatari ya kurudia tena vurugu kama lile liliozuka nchini mwanzo wa mwaka baada ya uchaguzi.

DPRK imeamua kuanzisha shughuli za viwanda vya nyuklia Yongbyon

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) yaani Mohamed ElBaradei aliripoti Ijumatatu kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Umma wa Korea (DPRK) au Korea ya Kaskazini, imeitaka IAEA kuondosha zile alama na vyombo vya upelelezi vilivyowekwa kwenye kiwanda cha nishati ya nyuklia katika mji wa Yongbyon, mtambo ambao ulifungwa mwaka jana.

MONUC yaripoti "utulivu dhaifu" warejea Kivu Kaskazini

Shirika la UM la Ulinzi wa Amani katika JKK (MONUC) limeripoti “utulivu dhaifu” umerejea katika jimbo la Kivu Kaskazini, hususan kwenye mji wa Sake, ambapo karibuni kulitukia mapigano makali kati ya vikosi vya Serikali (FARDC) na wafuasi wa kundi la waasi la CNDP.

Wakulima wadogo wadogo wanazingatiwa misaada ya kujitegemea

Hapa Makao Makuu leo asubuhi kulifanyika warsha kadha wa kadha juu ya masuala yanayohusu juhudi za kukuza maendeleo katika nchi maskini. Kwenye mkusanyiko mmoja kuliwasilishwa mradi mpya utakaofadhiliwa na wakf za kimataifa na kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kukuza pato na kujitegemea kimaisha.

Hapa na pale (Taarifa za kusoma)

Ripoti iliotayarsihwa bia na Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi wa Kimataifa (ILO), Shirika la Hifadhi ya Mazingira (UNEP), Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi wa Kimataifa na vile vile Shirika la Kimataifa la Waajiri inaashiria shughuli za kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa zikitekelezwa zina uwezo wa kuzalisha mamilioni ya fursa za ajira mpya itakayozozalisha “uchumi wa ajira ya kijani.” Mradi huu unatarajiwa kusaidia zile juhudi za kupunguza hewa chafu inayomwagwa angani yenye kuharibu mazingira, inayotokana na matumizi ya nishati ya petroli. Ripoti ilipewa jina la “Vibarua vya Kijani: Kuelekea Kwenye Kazi Stahifu Katika Ulimwengu Unaosarifika wenye Kaboni ya Chini.”

Mahojiano na M.Shirika, mwaathiriwa wa kunajisiwa kimabavu JKK

Mnamo mwezi Septemba Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), kwa ushirikiano na wanaharakati wa Marekani wanaogombania haki za wanawake wa jumuiya isiyo ya kiserikali inayoitwa V-Day, walitayarisha warsha maalumu katika majimbo ya Bukavu na Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) ziliopewa mada isemayo “Wanawake Wavunja Ukimya na Miko ya Kijadi” – tukio ambalo, kwa mara ya kwanza, kihistoria, wale wanawake walionusurika na ajali ovu ya kunajisiwa kimabavu, walipata fursa ya kuelezea mateso yao hayo hadharani. Kitendo hiki kilitaka ujasiri mkubwa, na lengo hasa lilikuwa ni kuwasaidia waathiriwa kuyapunga yale marohani yaliowasumbua kiakili ili waweze kupiga hatua ya kusonga mbele kimaisha.

Mahojiano na L. Sinai, mwaathiriwa wa pili wa mateso ya kijinsiya katika JKK

Mnamo mwezi Septemba Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF), kwa ushirikiano na wanaharakati wa Marekani wanaogombania haki za wanawake wa jumuiya isiyo ya kiserikali inayoitwa V-Day, walitayarisha warsha maalumu katika majimbo ya Bukavu na Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) ziliopewa mada isemayo “Wanawake Wavunja Ukimya na Miko ya Kijadi” – tukio ambalo, kwa mara ya kwanza, kihistoria, wale wanawake walionusurika na ajali ovu ya kunajisiwa kimabavu, walipata fursa ya kuelezea mateso yao hayo hadharani. Kitendo hiki kilitaka ujasiri mkubwa, na lengo hasa lilikuwa ni kuwasaidia waathiriwa kuyapunga yale marohani yaliowasumbua kiakili ili waweze kupiga hatua ya kusonga mbele kimaisha.~