Skip to main content

Uganda haiamini bei za juu za chakula ni tatizo, Raisi Museveni kuliambia Baraza Kuu

Uganda haiamini bei za juu za chakula ni tatizo, Raisi Museveni kuliambia Baraza Kuu

Kadhalika, kutoka Afrika Mashariki, Raisi Yoweri Museveni wa Uganda naye pia alishiriki kwenye majadiliano ya jumla ya kikao cha 63 cha Baraza Kuu.

"Kwa jinsi sisi tunavyohusika, hali hiyo tunaiona kuwa ni fursa halisi katika kadhia ya kukuza maendeleo. Hatuhisi kama ni kikwazo, hata kidogo! Kusema kweli, wakulima Uganda wanavuna pakubwa siku hizi .. na ndio maana tutaona uchumi wetu ulifanikiwa kukuwa kwa kiwango cha asilimia tisa kwa mwaka mnamo mwaka uliopita.”