Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raisi wa Kenya asema taifa limepiga hatua muhimu baada ya vurugu

Raisi wa Kenya asema taifa limepiga hatua muhimu baada ya vurugu

Majadiliano ya jumla ya Baraza Kuu (BK) la UM, kwenye kikao cha wawakilishi wote, yaliendelea mnamo alasiri ya siku ya mwanzo ya mahojiano ambapo Raisi Mwai Kibaki wa Jamhuri ya Kenya, alipohutubia mkutano, alisema nchi yake imepiga hatua muhimu kwenye maafikiano ya kurekibisha sheria, katiba na masuala mengine yanayaohitajika kutekelezwa ili kuepukana na na hatari ya kurudia tena vurugu kama lile liliozuka nchini mwanzo wa mwaka baada ya uchaguzi.

"Serikali inaitumia fursa hii ya kihistoria kuandaa makubaliano muhimu, yatakayotuwezesha kushughulikia yale masuala magumu yaliokabili taifa letu. Kwa mfano, tunafanya maendeleo ya kutia moyo kwenye juhudi za kuleta marekibisho, yenye natija za muda mrefu nchini, katika kurekibisha vyombo vya sheria, sera za kitaifa na pia katiba, hatua ambazo zitaimarisha zaidi mshikamano wa kitaifa, na kukidhi mahitaji ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ya umma wetu.”