Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na Pale

Hapa na Pale

Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio linaloitaka Iran kutekeleza, haraka, kwa ukamilifu yale maazimio yaliopita ya Baraza yalioshurutisha kusitishwa shughuli za kusafisha madini ya yuraniamu halisi inayotumiwa ama kuzalisha nishati ya umeme au silaha, na kuitaka ishirikiane nawakguzi wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA). ~~

Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (MONUC) limetuma platuni ya maofisa wa polisi 40 katika mji wa Goma, kusaidia vikosi vya polisi vya taifa kuendeleza sheria na utaratibu baada ya vurugu kuendelea kushtadi kwenye jimbo la Kivu Kaskazini. Vikosi vya taifa vya FARDC vimeshiriki kwenye mapigano makali katika wiki za karibuni na kundi la waasi la CNDP.

Waziri wa Taifa kwa Masauala ya Nchi za Kigeni wa Gambia, Omar Touray aliwaambia wajumbe wa kimataifa waliohudhuria mjadala wa Baraza Kuu wa wawakilishi wote kwamba mzozo wa chakula uliashiriwa kitambona nchi maskini, kwa sababu katika mwongo uliopita jamii ya kimataifa ilipuza kabisa huduma za kilimo kwenye nchi zinazoendelea. Alisema katika kipindi hicho shughuli za utafiti wa kuendeleza kilimo pamoja na taasisi za mafunzo zilivurugika kijumla, na kuzorota kwa sababu ya ukosefu wa misaada ya fedha kutoka kwa wahisani wa kimataifa. Alisema umma wa nchi zinazoendelea waliona soko zao za kilimo zikiangamia baada ya kumezwa na bidhaa za nchi zenye maendeleo ya viwanda, ambapo wakulima wa huko hufadhiliwa ruzuku na serikali zao inayowasaidia kuendesha shughuli za kilimo bila matatizo. Waziri Touray alipendekeza wakulima wa mataifa yanayoendelea wasaidiwe na jumuiya ya kimataifa, kwa hali na mali, kukuza uwezo wao wa kushindana kuzalisha bidhaa za kilimo zenye thamani ili kuvuna natija za biashara kwenye soko la kimataifa.