Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Hafla ya kusoma kitabu cha mstaafu rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete chuo cha New York, Marekani
UN News Kiswahili/Anold Kayanda

Baada ya jando ndio nilipatiwa viatu- Dkt. Kikwete

Kwa mara ya kwanza nilivaa viatu baada ya kutoka jandoni, ni kauli ya Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyotoa wakati akizungumzia kilichomo kwenye kitabu chake Safari yangu kutoka mwanafunzi aliyekwenda shule peku hadi Urais, kitabu kitakachozinduliwa hivi karibuni.

Familia ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa 7 wa UN Kofi Annan, ikiwa imezunguka jeneza lake kabla ya mazishi mjini Accra, Ghana hii leo tarehe 13 Septemba 2018
UN News/Ben Malor

Sasa nimetambua upekee wa Annan- Guterres

Tangu kifo cha Kofi Annan, nimekuwa nikitafakari ni kitu gani kilimfanya awe wa kipekee! Hivi ndivyo ambavyo Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewaeleza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mmoja wa watangulizi wake Kofi Annan aliyezikwa leo huko Accra nchini Ghana. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.