Vikosi vya Umoja wa Mataifa Sudan Kusini vinawapeleka wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.
Walinda amani Sudan Kusini wasindikiza wanafunzi shuleni na kuwarudisha nyumbani wakati wa mitihani.Polisi waliopo kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini wamepewa jukumu la kuwasindikiza wanafunzi hadi kwenye kituo cha mtihani kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Usindikizaji huo unafanyika Kwa wiki mbili ambapo askari hao wataendelea kuwapeleka na kuwarudisha wanafunzi kufanya mitihani yao kwa usalama.