Asafiri kutoka Venezuela hadi Chile kwa mguu akiwa mjamzito, sasa anaona nuru
Huko Amerika ya Kusini Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unaendelea kusaidia wahamiaji wanaokimbia ghasia na changamoto kwenye nchi zao.
Huko Amerika ya Kusini Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unaendelea kusaidia wahamiaji wanaokimbia ghasia na changamoto kwenye nchi zao.
Kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupitia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo - MONUSCO wamehitimisha kampeni yao ya Afya na Amani iliyoanza tarehe 3 mwezi huu wa January ambapo wamekabidhi jengo kwa ajili ya mahali pa wagonjwa na wahudumu wa afya kula chakula katika Kituo cha Afya cha Mavivi, mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali shambulio lililotokea jana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa moja huko Kasindi, jimboni Kivu Kaskazini. Selina Jerobon anaarifu zaidi.
Wananchi wa eneo la Potopoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, wameeleza furaha yao baada ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha 6 cha Tanzania kinachohudumu nchini humo chini ya MINUSCA, kutumia wataalamu wake wa afya kutoa matibabu na dawa katika Zahanati ya Potopoto wilayani Mambéré-Kadéï.
Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu kesi iliyoanza huko Lesvos nchini Ugiriki dhidi ya watetezi 24 wa haki za binadamu wanaoshtakiwa kwa kutekeleza jukumu la kuokoa wahamiaji ambao walikumbwa na zahma baharini wakati wakikimbilia barani Ulaya kusaka maisha bora. Kesi hiyo imeanza wiki hii baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu.
Katika kusaidia jamii hususan za vijijini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Somalia linatekeleza mradi wa kisasa wa kuvuna na kuhifadhi maji ili kuweza kuwasaidia wananchi wa vijiji vitatu ambao wanajishughulisha na kilimo na ufugaji.
Uganda hii leo imetangaza kutokomeza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliosababishwa na virusi aina ya Sudan, ikiwa ni chini ya miezi minne tangu kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza kwenye wilaya ya Mubende nchini humo 20 mwezi Septemba mwaka jana. Taarifa ya Thelma Mwadzaya inafafanua zaidi.
Nchini Rwanda Umoja wa Mataifa unashirikiana na serikali kuimairisha huduma za uzazi ili hatimaye kuhakikisha kila uzazi unakuwa salama si tu kwa mama bali pia mtoto anayezaliwa. Kupitia mradi uliofadhiliwa na TAKEDA, kampuni hii ya utafiti na dawa duniani, Rwanda imeweza kuimarisha huduma kwenye hospitali na vituo vya afya.
Tarehe 24 mwezi huu wa Januari ni siku ya elimu duniani ikimulika mafanikio na changamoto za kufanikisha lengo namba 4 la kufanikisha elimu bora kwa kila mtu kokote aliko. Elimu bora ni pamoja na vifaa vya ikiwemo madaftari, vitabu na kalamu ambako kwa watoto wengine bado vinasalia kuwa anasa.
Kikosi cha 9, TANZBATT 9 cha wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo DRC-MONUSCO, wameendelea na kampeni yao ya Afya na Amani ambapo hadi tarehe 13 mwezi huu wa Januari watakuwa wakiendelea kutoa misaada kwa jamii inayoishi katika eneo lao la kazi, kaskazini mashariki mwa nchi.