Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kuvuna maji ya mvua kuwanufaisha wakulima na wafugaji wa Somaliland

Sand dams huko Puntland, Somalia, yanaweza kuvuna maji kutoka juu na pia chini ya ardhi na kusaidia kujenga ustahimilivu wa watu wa eneo hilo. (Maktaba)
UNDP Somalia/Said Isse
Sand dams huko Puntland, Somalia, yanaweza kuvuna maji kutoka juu na pia chini ya ardhi na kusaidia kujenga ustahimilivu wa watu wa eneo hilo. (Maktaba)

Mradi wa kuvuna maji ya mvua kuwanufaisha wakulima na wafugaji wa Somaliland

Tabianchi na mazingira

Katika kusaidia jamii hususan za vijijini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Somalia linatekeleza mradi wa kisasa wa kuvuna na kuhifadhi maji ili kuweza kuwasaidia wananchi wa vijiji vitatu ambao wanajishughulisha na kilimo na ufugaji.

Katika kusaidia jamii hususan za vijijini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Somalia linatekeleza mradi wa kisasa wa kuvuna na kuhifadhi maji ili uweza kuwasaidia wananchi wa vijiji vitatu ambao wanajishughulisha na kilimo na ufugaji.

Wakulima na wafugaji wa maeneo ya Qardho, Puntland na Xabaale huko Somaliland kwa miaka mingi walikuwa wakitegemea maji kutoka visimaji ili kuweza kuendeleza shughuli za kilimo na ufugaji lakini gharama kubwa za kuvuta maji kisimani kwakutumia jenereta ziliwawia vigumu kuendesha shughuli zao za kuwapatia kipato hususan wakati wa kiangazi.

Ni kutokana na changamoto hiyo, FAO nchini Somalia chini ya ufadhili wa Muungano wa Ulaya ikaanzisha programu ya usimamizi wa maji na ardhi ijulikanayo kama SWALIM- yani Somalia Water and Land Management ambapo kwa kushirikiana na viongozi wa maeneo hayo matatu, watunga será na wadau wa taasisi nyingine wakaanzisha mradi wa kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi katika mabwawa madogo yaliyochimba pamoja na matanki ya maji na ili kupunguza gharama, utuaji wa maji hayo sasa utafanyika kwa nishati ya jua, yani umeme wa Sola. 

FAO pia imetoa mafunzo ya ukulima bora unaozingatia mabadiliko ya tabianchi na matumizi bora ya maji kwa wana jamii na kisha kutoa vifaa vya umwagiliaji kwa kaya 4700 ambazo sasa zipo tayari kuboresha maisha yao kama anavyoeleza Nasma Baadri Aw Mohamed, mkulima huko Xabaale

Nasma Baadri Aw Mohamed- Mkulima wa Xabaale anasema, “Tunasubiria kwa hamu mradi huo wa kuvuna maji ukamilike. Tutaweza kumwagilia mashamba yetu, kupanda mboga za majani katika mashamba yetu na pia maji yakiwa yanapatikana katika maeneo yetu mifugo yetu itapata maji ya kutosha, kitu ambacho walikuwa wanakosa hapo awali”

Mbali na kuwawezesha wananchi, Afisa rasiliamli ardhi wa FAO Ali Ismail Ibrahim anasema

Ali Ismail Ibrahim, Afisa rasiliamli ardhi wa FAO anasema“Malengo ya mradi huu ni kuwajengea uwezo watendaji wa serikali kwenye maeneo ya ardhi na maji na pia tumeanzisha kituo cha usimamizi wa taarifa”

Tayari vituo viwili vimeanzishwa huko Puntland na Somaliland na vina wafanyakazi wa kujitolea waliopewa mafunzo na FAO ili kusaidia usimamizi bora wa rasilimali za ardhi na maji.

Mkurugenzi wa kituo cha Puntland Abdinur Ali Jama anasema …

Abdinur Ali Jama, Mkurugenzi wa kituo cha Puntland anasema, “Kituoni hapa tunatoa taarifa zihusianazo na utabiri wa mvua, ukame na usimamiz wa taarifa za ukame katika eneo hili“.