Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya Mavivi, walinda amani wa UN kutoka Tanzania wafikisha misaada Hospitali ya Oicha, DRC

Walinda amani kutoka Tanzania waanzisha kampeni ya "Afya na Amani" nchini CRC
Picha: MONUSCO
Walinda amani kutoka Tanzania waanzisha kampeni ya "Afya na Amani" nchini CRC

Baada ya Mavivi, walinda amani wa UN kutoka Tanzania wafikisha misaada Hospitali ya Oicha, DRC

Amani na Usalama

Kikosi cha 9, TANZBATT 9 cha wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo DRC-MONUSCO, wameendelea na kampeni yao ya Afya na Amani ambapo hadi tarehe 13 mwezi huu wa Januari watakuwa wakiendelea kutoa misaada kwa jamii inayoishi katika eneo lao la kazi, kaskazini mashariki mwa nchi.

Walianza na Kituo cha afya cha Mavivi na sasa ilikuwa zamu ya Hospitali ya Oicha katika mji wa Beni.

Taarifa ya Kapteni Denisia Lihaya ambaye ni Afisa habari wa Kikosi hicho inaanza na maelezo ya Meja Frank Mtwanzi aliyekabidhi msaada huo kwa niaba ya Kamanda wa Kikosi.

Akikabidhi dawa hizo kwa niaba ya Kamanda kikosi cha TANZBATT 09 Meja Frank Mtwanzi amesema lengo kuu kampeni na kukabidhi dawa hizo katika Hospitali ya Oicha ni kuendeleza uhusiano ulipo baina ya walinda Amani kutoka Tanzania na wananchi katika eneo la uwajibikaji.

Naye Fabrice Maboko’ mfamasia Hospitali ya Oicha, akipokea dawa hizo amesema,

Kwa upande wake Mfamasia wa Kikosi cha tisa cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania Kopolo Victoria Riwa amesisitiza kuwa dawa hizo zitasaidia jamii ya wanawake na watoto kwani ndio waathirika wakubwa katika maeneo yenye changamoto za kiusalama.

Akitoa maoni yake kuhusu msaada huo mtaalamu wa Saikolojia wa kituo Afya cha Mavivi, Mama Augene amesema,