Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Katika kituo cha ukusanyaji wa pamba Brazil ambako pamba hutenganishwa na mbegu kabla haijashindiliwa na kuhifadhiwa
FAO/Alberto Conti

Pamba, kitambaa kinachositiri  zaidi ya familia milioni 100 duniani:UN

 Leo ni siku ya pamba duniani ikiwa ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku hiyo kuenzi zao ambalo kitabaa chake kinatengeneza mavazi ya kila siku yaliyosheheni kwenye mkabati mengi ya nguo na ni kitambaa kizuri, rahisi kuvaa, kukitunza na kinadumu kwa muda mrefu. Lakini kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa thamani ya pamba ni zaidi ya kitambaa kama inavyofafanua taarifa ya Flora Nducha 

Sauti
2'40"
Mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani katika sekta ya uvuvi umepelekwa pia mkoani Katavi kusini-magharibi mwa Tanzania.
UN Tanzania

Kutoka Kigoma, mradi wa FISH4ACP wahamishiwa mkoani Katavi 

Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo duniani, FAO limetambulisha mradi wa FISH4ACP wa kuongeza mnyororo wa thamani ya mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika mkoani Kigoma baada ya mradi huo unaohusisha nchi 12 za Afrika, Karibea na Pasifiki kuwa na matokeo chanya kwa wavuvi mkoani Kigoma. Devotha Songorwa wa Radio washirika KidsTime FM anafafanua zaidi katika ripoti hii. 

Sauti
4'27"
Gwaride la walinda amani wa Tanzania nchini DRC kabla ya kutunukiwa  nishani za Umoja wa Mataifa
Kapteni Tumaini Bigambo

Walinda amani wa Tanzania nchini DRC watunukiwa nishani za Umoja wa Mataifa

Walinda amani kutoka Tanzania, Kikosi cha 8 cha kujibu mashambulizi kinachohudumu katika ulinzi wa amani chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, FIB MONUSCO wametunukiwa nishani ya Umoja wa Mataifa katika sherehe zilizopambwa kwa gwaride maalum lililoandaliwa na kikosi hicho. Afisa habari wa TANZBATT8, Kapteni Tumaini Bigambo alikuwepo katika hafla hiyo ana ametuandalia ripoti ifuatayo.

Sauti
2'36"
Wasichana wakicheza kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani nje ya mji wa Herat Afghanistan
© UNICEF/Sayed Bidel

Utapiamlo kwa watoto umefurutu ada Afghanistan:UNICEF/WFP 

Hali ya kutokuwa na uhakika wa chakula na vita nchini Afghanistan vimeongeza mara dufu tatizo la utapiamlo kwa watoto na kuzusha wasiwasi mkubwa kwa hatama ya watoto hao na familia zao yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP ambayo sasa yametoa wito wa mshikamano kunusurua taifa hilo.

Sauti
2'26"
UNMAS wakitegua mabomu katika eneo la Equatoria mashariki nchini Sudan Kusini. Pichani ni eneo shambani ambako kilipuzi kimebainika
UNMISS\Nektarios Markogiannis

Mabaki ya silaha za vita yaliyozagaa Sudan Kusini ni tishio kubwa la usalama wa raia:UNMAS 

Nchini Sudan Kusini wakati sasa milio ya risasi inaweza kuwa imepungua katika baadhi ya maeneo ya taifa hilo, jinamizi la vita vya wenyewe kwa wenyewe bado linawaandama hasa kwa kuzagaa kwa manbaki ya silaha za vita kama mabomu ya kutegwa ardhini na vifaa vingine vya mlipuko, ambavyo kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayochukua hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS ni tishio la kila siku kwa maisha ya wanawake, watoto na wanaume kwenye maeneo mbali mbali nchini humo 

Sauti
2'11"