Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mafunzo ya FAO mkoani Kigoma yamewezesha wanakikundi kutumia viazi lishe kutengeneza juisi, na kupika maandazi, chapati na kukaanga chipsi.

Viazi lishe Kenya ni zaidi ya chakula ni mkombozi wa maisha:WFP

FAO Tanzania
Mafunzo ya FAO mkoani Kigoma yamewezesha wanakikundi kutumia viazi lishe kutengeneza juisi, na kupika maandazi, chapati na kukaanga chipsi.

Viazi lishe Kenya ni zaidi ya chakula ni mkombozi wa maisha:WFP

Ukuaji wa Kiuchumi

Programu ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini Kenya kuzalisha, kupika na kuuza viazi vitamu au viazi lishe imeleta nuru hasa kwa wanawake ambao sasa wanaweza kukimu mahitaji ya familia zao na kujiongezea kipato

Video ya WFP inaonesha mmoja wa wanawake wakulima wadogo na wafaidika wa mradi wa WFP akisema viazi lishe vinaweza kutumika kwa mambo mengi ikiwemo kutengeneza vitafunwa, chips, na hata kuchanganya kwenye mapishi ya chapati.

WFP inasema mradi huo wa viazi lishe ni zaidi ya chakula watu wanachokula kwani pia unawasaidia wakulima kwenda sanjari na mabadiliko ya tabianchi , kuboresha lishe ya jamii zao na kujiongezea kipato na wakulima wengi wamejiunga katika vikundi ili kusaidia 

“Tuna wanawake 18 na wanaume 12 kwenye kundi letu, kutokana na mavuno yetu ya viazi vitamu wanachama wote hawa wanaweza kulisha watoto wao” 

Kwa mujibu wa WFP viazi hivi ambavyo vina rangi ya machungwa vinahimili ukame na changamoto zingine za mabadiliko ya tabianchi, lakini pia gharama yake ni nafuu hali ambayo inaongeza neema kwa wakulima hawa wadogo wa Kenya. 

“Vina thamani kubwa ya lishe hivyo tunafurahi sana tunapovila au kuviuza kwa sababu tunapata fedha za kusomesha watoto wetu” 

Kwa mantiki hiyo WFP inasema viazi lishe ni muhimu sana hasa kwa mifumo ya chakula ya Kenya.