Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Baadhi ya maeneo ya Niger yameharibiwa kutokana na matumizi mabaya ya ardhi yasiyo endelevu.

Mradi wa Benki ya Dunia Niger waleta nuru kwa wakulima na wafugaji

©FAO/Giulio Napolitano
Baadhi ya maeneo ya Niger yameharibiwa kutokana na matumizi mabaya ya ardhi yasiyo endelevu.

Mradi wa Benki ya Dunia Niger waleta nuru kwa wakulima na wafugaji

Tabianchi na mazingira

Nchini Niger, mradi wa Benki ya Dunia wa hatua za kijamii za kuchukua hatua kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi, PACRC umesaidia jamii kuweza kutumia mbinu mpya mbunifu na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi,

Katika taifa la Niger ambalo ni moja ya mataifa yaliyoko ukanda wa Sahel, tishio la athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri. Viwango vya joto ni mara 1.5 kuliko kwenya maeneo mengine ya dunia.  

Ukame, mafuriko na mmomonyoko wa udongo ni sababu za sekta ya kilimo kupoteza ardhi yenye rutuba na hivyo kuathiri uhakika wa wanchi kuwa na uhakika wa chakakula .

Zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa Niger wanategemea kilimo na wengi wao ni wakulima wa kiwango kidogo na hivyo kuamuliwa kupatiwa msaada kupitia mradi wa Benki ya Dunia ambapo Taibatou Issa ambaye ni mmoja wa rais wa vikundi nufaika wa mradi huo anasema, “Kabla kuanza kwa mradi nillazimika kufanya biashara nyingi ndogo ndogo. Haikuwa rahisi."

Jumba la wakulima, ni fursa kwa wakulima na watoaji  huduma za kiufundi za killmo wanakutana kujadili mifuko ya mikopo ya pembejeo, kilimo na ustawi.  

Halikadhalika wakulima na wafugaji wanapata mbinu za kufuga mifugo, kilimo bora na pia kilimo cha umwagiliaji maji kwa matone. Taibatou anasema, “kupitia jumba la wakulima niliweza kupata chakula cha mifugo, huduma hii imepunguza gharama, kwa kuwa awali ilikuwa gharama kubwa sana kwangu.” 

Mradi huo umeenda mbali zaidi ambapo Nassour Cheia kutoka Niger anasema “Jumba la wakulima linasaidia pia kuleta wakulima pamoja na pia kupata mbegu za kisasa zinazostahimili ukame. Mbegu hizo ni bora kuliko zile za asili.” 

Sasa wakulima wana matumaini makubwa kwa kuwa wamepatiwa mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji na hivyo kuwa na uhakika wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika ukanda wa Sahel. 


TAGS; Sahel, Niger, Mabadiliko ya Tabianchi