Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya, Abenyo Natiir  (kati- kulia) akitengeneza shanga za urembo akiwa na binti yake Awesit Lisilgor (kushoto- kati)
© UNICEF/Nichole Sobecki

Katikati ya ukame Pembe ya Afrika, bado kuna tumaini la nuru ya kujikwamua

Pembe ya Afrika hali ya ukame inazidi kutishia uwezekano wa baa la njaa kwenye eneo hilo linalojumusha Kenya, Somalia na Ethiopia huku Umoja wa Mataifa ukisema takribani watu milioni 18.4 huamka kila siku bila uhakika wa mlo huku idadi hiyo ikitarajiwa kufikia milioni 20 mwezi ujao wa Septemba. Wanawake na watoto wameathirika zaidi ambapo kando ya njaa wanakumbuka kile walichokuwa wanafanya hali ilivyokuwa nzuri na wanatamani hali hiyo irejee.

Sauti
2'24"
Chanjo dhidi ya malaria katika kituo cha afya.
GAVI

Mamilioni ya watoto kunufaika na chanjo ya Malaria

Kampuni ya kutengenza dawa za binadamu ya GSK imepatiwa kandarasi ya kuzalisha chanjo ya kwanza ya Malaria duniani lengo likiwa ni kulinda mamilioni ya watoto dhidi ya ugonjwa huo unaogharimu mamilioni ya Maisha ya watoto limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF hii leo. 

Mwelekeo wa shehena za vyakula kutoka Ukraine.
UN News

Hatimaye meli yenye shehena ya ngano yaondoka Ukraine kuelekea Pembe ya Afrika

Meli ya kwanza ya Ukraine yenye na unga wa ngano wa Ukraine utakaosambazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP kwenye operesheni zake za kibinadamu imeondoka bandari ya Yuzhny nchini Ukraine hii leo,  hatua ambayo imetajwa kuwa ya muhimu zaidi na inayohitajika ya kuondoa nafaka kwenye taifa hilo lenye mzozo kuelekea nchi zinazokumbwa na janga la uhaba wa chakula duniani. 

Kituo cha uwezeshaji wanawake kwenye mji mkuu wa Afghanistan, Kabul
UN Afghanistan

Mwaka mmoja wa watalibani Afghanistan, sera dhahiri za ukosefu wa usawa zashamiri

Mwaka mmoja tangu watalibani watwae madaraka nchini Afghanistan, shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake duniani, UN-Women hii leo limesihi mamlaka hizo kufungua shule kwa ajili ya watoto wote wa kike, ziondoe vikwazo vya ajira kwa wanawake na ushiriki wao kwenye siasa za taifa hilo sambamba na kufuta sera zote zinazowanyima wanawake na wasichana haki zao.

Sauti
3'15"