Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hali ilivyo katika maeneo ya kushikilia wahamiaji na wasaka hifadhi. Hapa ni Libya nje kidogo ya mji mkuu, Tripoli.
UNICEF/Alessio Romenzi

Pengo la huduma za ulinzi safari latumbukiza wakimbizi mikononi mwa wasafirishaji haramu

Kuelekea siku ya kimataifa dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu kesho Julai 30, shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi duniani, UNHCR imesema ukosefu wa huduma za ulinzi kwa wakimbizi na wahamiaji wanaofanya safari hatarishi kutoka ukanda wa Sahel na Pembe ya Afrika kwenda Afrika Kaskazini na kisha Ulaya, kunawatumbukiza katika hatari ya mikono ya wasafirishaji haramu. 

Sauti
2'23"
Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi Tanzania
UN News

FAO Tanzania yazindua tawi la Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA

Katika kutekeleza lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu ajira za staha na ukuaji kiuchumi sambamba na namba 5 la usawa wa kijinsia, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo duniani FAO nchini Tanzania,  limezindua tawi la tatu la Mtandao wa Wanawake Wanaojihusisha na Shughuli za Uvuvi TAWFA kupitia mradi wake wa kukuza mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi katika ziwa Tanganyika.

Sauti
4'19"