Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu huru wa haki za binadamu ziarani nchini Mali

Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa nchini Mali Alioune Time
UN Geneva/Aurore Bourdin
Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa nchini Mali Alioune Time

Mtaalamu huru wa haki za binadamu ziarani nchini Mali

Haki za binadamu

Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Mali, Alioune Tine, anatarajia kuanza ziara ya wiki mbili nchini Mali kuanzia tarehe 1 hadi 12 mwezi Agosti 2022.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu kutoka Geneva Uswisi imemnukuu Tine akisema “Ziara hii itaniruhusu kuendelea na tathmini ya jumla ya hali ya haki za binadamu nchini Mali na kuunga mkono mamlaka ya mpito ya nchi hiyo katika jitihada zao za kukuza na kulinda haki za binadamu, pamoja na kuhakikisha utekelezaji wake.”

Mtaalamu huyo katika ziara yake anatarajia kukutana na mamlaka za umma ili kujadili hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa ahadi nilizotoa kwenye mapendekezo ya awali “hususan katika mapambano dhidi ya kutokujali”. 

Mbali na mamlaka za umma pia akiwa mjini Bamako na maeneo mengine anatarajia kukutana na jumuiya za kiraia na waathirika, mashirika yasiyo ya kiserikali, wanadiplomasia na mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyomo nchini Mali.

Baada ya ziara hiiyo Tine atawasilisha ripoti yake ya kila mwaka kwa Baraza la Haki za Kibinadamu mnamo Machi 2023.