Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Somalia

Tarehe 24 Aprili 2017, mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya surua huko kambini Beerta Muuri mjini Baidoa nchini Somalia.
UNICEF/Yasin Mohamed Hersi

Kuna dalili za ‘kimbunga’ cha mlipuko wa Surua: WHO/UNICEF

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia watoto, UNICEF na la afya duniani, WHO yamesema idadi ya wagonjwa wa surau duniani kwa miezi miwili ya mwanzo ya mwaka huu wa 2022 imeongezeka kwa asilimia 79 kulinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana na hivyo kuwa ni mazingira yanayoweza kuchochea mlipuko wa ugonjwa huo unaozulika kwa chanjo.

Bi. Joyce Msuya, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN na Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA katika mahojiano na UN News Kiswahili Aprili 2022 New York, Marekani.
UN/ Anold Kayanda

Ukame Pembe ya Afrika: UN katu haiwezi kusahau licha ya majanga mengine duniani

Licha ya majanga mengine ya kibinadamu yanayoendelea duniani ikiwemo kule Ukraine, bado Umoja wa Mataifa unahangaika kila uchao kuhakikisha inasaidia wakazi wa Pembe ya Afrika ambako ukame umesababisha watu milioni 15 kukosa uhakika wa chakula, amesema Joyce Msuya Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya dharura, OCHA.

 

Mtoto mwenye umri wa miezi 7 akichnguzwa utapiamlo unaochochewa na ukame mkali nchiin Somalia.
© UNICEF/Sebastian Rich

Janga la njaa lanyemelea Somalia- UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa janga lingine la njaa kama la mwaka 2011 linanyemelea Somalia iwapo wahisani hawataongeza ufadhili wao kwa ombi la usaidizi wa kibinadamu kwa taifa hilo la pembe ya Afrika kwa kuwa ukame wa muda mrefu sambamba na ongezeko la bei za vyakula vimeongeza idadi ya wasio na uhakika wa chakula kufikia watu milioni 6, sawa na asilimia 40 ya wananchi wote. 

Sauti
1'58"
Ahmad Hassan Yarow mwenye umri wa miaka 70 katika kambi ya wakimbizi wa ndani Luuq nchini Somalia
UN Photo/Fardosa Hussein

Katika umri wangu wa miaka 70 sijashuhudia ukame wa kiwango hiki- Mwananchi Somalia

Akiwa amesimama mbele ya kibanda chake kwenye makazi ya wakimbizi ya Kulmiye wilayani Luuq nchini Somalia, Ahmad Hassan Yarrow anatazama kile kilichosalia katika mto Juba, ambao ulikuwa ndio tegemeo la uhai wa  eneo lao. Mto umekauka. “Katika umri wangu wa miaka 70 sijawahi kushuhudia ukame kama huu, katika vipindi vyote vya ukame vilivyopita,” anasema Bwana Yarrow katika makala iliyochapishwa kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM.

Sauti
3'4"