Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndoto yangu kusakata gozi la kulipwa haikutimia lakini sasa naitimiza kwa wengine: Aweys Haji Nur 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Ndoto yangu kusakata gozi la kulipwa haikutimia lakini sasa naitimiza kwa wengine: Aweys Haji Nur 

Masuala ya UM

Kama iliyo kwa wavulana wengi duniani, Aweys Haji Nur kutoka Somalia alipokuwa mdogo alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasoka wa kulipwa. 

Hata hivyo, wakati haukuwa muafaka, alizaliwa mwaka 1984, ambayo inamaanisha kuwa ujana wake ulighubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka mwaka wa 1991 na kusambaratisha sehemu kubwa ya Somalia katika kipindi cha miaka 30 iliyofuata. 

Kwa hivyo Bwana Nur alibidi aziweke ndoto zake za umaarufu na utukufu kwenye uwanja wa mpira kabatini, na kutafuta riziki katika uwanja mwingine. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Alizaliwa na kukulia Mogadishu, na Nur alisoma shule ya msingi na sekondari ya Tadamun, na kuendelea na elimu yake ya juu ya sekondari katika shule ya upili ya Usama Bin Zeyd.  

Baada ya hapo akaendelea na masomo ya elimu ya juu, na kumaliza shahada ya kwanza katika tasnia ya sayansi ya siasa na Habari katika chuo kikuu cha Mogadishu mwaka 2013. 

Hakuishia hapo akasoma pia shahada ya uzamili ya utawala wa biashara ya kimataifa katika chuo kikuu cha Amity, nchini India, kupitia elimu ya masafa marefu kwa njia ya mtandao, kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.  

Kisha akapata kazi yenye mafanikio makubwa kama mwanahabari mkuu na mkurugenzi wa habari wa vyombo vya habari vya Somalia vinavyojulikana kama Horn-Afrik na Mustaqbal Media, miongoni mwa vingine. Kwa sasa yeye ni mkurugenzi wa Goobjoog TV nchini Somalia. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Ndoto za kandanda 

Lakini, licha ya mafanikio yake katika sekta ya habari, ndoto yake Nur ya soka haikumwacha kabisa. 

Katika muda wake wa mapumziko, anafuatilia soka kwa bidii kama burudani na, mara kwa mara, anajitolea kuwafundisha wavulana wa huko Mogadishu ambao wanatamani kuwa wachezaji wa kandanda. 

“Kila nilipowaona wavulana wakicheza mbele ya nyumba yangu, nilijiona kama mtoto na ilinihuzunisha. Bado hatuna fursa za kutosha kwa watoto kuwawezesha kutimiza ndoto zao, niliona jinsi ambavyo wangeweza kufikia ndoto zao kama wangekuwa na mtu wa kuwasaidia," anasema Bwana Nur, ambnaye sasa ni baba wa watoto saba. 

Ameongeza kuwa “Nadhani watoto wa Somalia wana bahati mbaya kuliko watoto wa sehemu zingine duniani, kwa sababu hawana mazingira salama na muafaka ya kuendeleza ujuzi wao wa kusakata kabumbu.” 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kambumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kambumbu kesho.

Akijaribu kuangalia njia za kuwasaidia watoto hao Nur, alibaini kuwa hakukuwa na mfumo rasmi wa kukuza vipaji vya soka kwa vijana nchini Somalia na hakuna aliyeonekana kuwa na nia ya kuanzisha mfumo, hasa kutokana na kuzingatia kuwa nchi hiyo iko katika mchakato wa kujijenga upya baada ya miongo kadhaa ya migogoro. 

Akiwa amechoka kungoja na hakuweza kuondoa kabisa shauku yake kwa mchezo huo maridhawa Nur aliamua kubeba jukumu mikononi mwake. 

Mnamo 2018, alifungua chuo cha soka cha ITAAL, ambacho ni kituo cha mafunzo kwa vijana wenye matarajio kama aliyokuwa nayo yeye ya kusakata gozi la kulipwa. 

"Nilianzisha ITAAL Academy ili kutimiza ndoto za watoto," anasema Nur kwa fahari. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Wanafunzi wawili wa kwanza wa chuo hicho walikuwa wana wawili wa Bwana Nur. Hivi sasa, kuna wavulana 30 waliojiandikisha katika chuo hicho.  

Chuo hicho kipo katika wilaya ya Wadajir mjini Mogadishu na kinajumuisha uwanja wa michezo na ofisi ndogo, kikihudumia watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi na moja, na uandikishaji huamuliwa sio tu na afya na stamena ya kusakata kandanda na uwezo wa mgombea bali pia na shauku yao kwa mchezo. 

Chuo ni cha bure hakitozi ada. Bwana Nur anatumia pesa zake mwenyewe kufadhili shughuli za kila siku za chou hicho, na mara kwa mara hupokea usaidizi kutoka kwa marafiki ambao wanashiriki mapenzi yake ya soka na kutaka kuwasaidia vijana wa Somalia. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Bwana Nur hajajikita tu upande wa utawala wa chou, pia anaenda uwanjani kama mmoja wa wakufunzi wake.  

Kwa upande huo alipata cheti chake kama mkufunzi wa kandanda ya vijana kutoka Shirikisho la Kimataifa la Soka duniani (FIFA) mwaka 2021. 

Tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyopita, timu za ITAAL Football Academy zimehudhuria mashindano manne yanayotambuliwa na shirikisho la soka la Somalia (SFF) na matatu kati ya hayo walishinda.  

Wachezaji wa chou hicho pia walishiriki katika mashindano ya FIFA Grassroots huko Mogadishu mwezi Oktoba 2021. 

Mtandao wa soka 

Ili kuwa na chaguo kwa wachezaji wachanga wenye vipaji ambao wanaweza kuendeleza uwezo wao, Bwana Nur alianzisha uhusiano na mamlaka ya soka ya Somalia na baadhi ya vilabu nchini Somalia na nje ya nchi. 

"Tuna uhusiano mzuri na shirikisho la soka la Somalia, na pia tuna uhusiano mzuri na vilabu vya soka ndani na nje ya nchi, kama vile Som United ya Uswis, na klabu za Ligi kuu ya Somalia Wahol, Elman, na Mogadishu City," anasema Nur. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

 Shirikisho la soka la Somalia halina kingine ila sifa kemkem kwa juhudi za Bwana Nur, likizielezea kama hatua muhimu katika kuendeleza uwanja wa soka nchini humo. 

"Shirikisho la soka la Somalia linaona juhudi za Aweys kama kijana anayetayarisha wachezaji wachanga ambao tunaamini wataifaidisha nchi na kuunda uti wa mgongo wa maendeleo ya soka. Naamini juhudi zake zitaboresha soka la Somalia," anasema mkurugenzi wa masuala ya ufundi wa SFF, Awil Ismail Mohamed. . 

Bwana Mohamed anaendelea kusema "Tunamhimiza kuendeleza kazi hii nzuri, kuna ushirikiano uliopo kati yetu na Aweys, na Shirikisho linaunga mkono bila masharti watu kama Aweys katika kujitolea kusaidia watoto wa Somalia wanaohitaji sana mafunzo ya kutegemewa ya michezo." 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Wazazi wa wanaofunzwa katika Chuo cha Soka cha ITAAL wanakubali. 

"Ninaona fursa hii kama ya kufurahisha na ya elimu kwa sababu ni sehemu chache kama hizo ambapo watoto huendeleza ujuzi wao na vipaji vyao wakati wa likizo ya shule, hii imesaidia watoto wangu kuepuka kucheza mitaani ambako walikuwa hatarini zaidi au kwenda sehemu za mbali na ambako wanaishi. Ni vigumu kuwaangalia, na ninaamini hii ni fursa ambayo tumekuwa nayo na ninapendekeza iongezewe," anasema Sultana Mohamed, mama wa wavulana wawili waliosajiliwa katika chuo hicho. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Sifa kemkem 

Nur anasema sifa ambayo chuo cha soka cha ITAAL kinaifurahia imeongezeka tangu kuanzishwa kwake. 

“Wazazi wanawasiliana nami kila mara na kuomba mtoto wao aandikishwe katika chuo hicho, jambo ambalo linanifurahisha,” anabainisha. 

Lakini licha ya kusifiwa na kutambulika, ili kuhakikisha kwamba uwezo wa chuo hicho unakuwa mkubwa si jambo rahisi na, licha ya kuungwa mkono na baadhi ya maeneo, bado ni ushuhuda  mkubwa wa kujitolea na shauku ya Bwana Nur. 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

"Kwa sasa, sina mtu wa kuniunga mkono. Natumia sehemu ya mshahara wangu kwenye soka, na kuna watu binafsi au vilabu ambavyo wakati mwingine hutoa mipira au vifaa vya michezo," Anasema Nur  

"Tuna chaguzi chache za nafasi za mafunzo. Hatuna fursa ya kufikia viwanja vya kujitegemea vya kufanya mazoezi kwa saa nyingi, na kwa hivyo inatubidi kuvikodisha,” anaendelea. “Hatuna pesa nyingi; tunakodisha kwa saa chache tu, na hiyo haitoshi. Pia, kwa vile ni watoto, tunapofika na kutoka viwanjani, tunalazimika kuwasafirisha kwa basi, na pia tunalazimika kulipia gharama hizo.” 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

Bwana Nur ana matumaini kuhusu kupata usaidizi zaidi kwa chuo hicho. Wakati huo huo, anasema anasalia kuwa mwanasoka moyoni, na amejitolea kusaidia kukuza Wasomali vijana wa leo kuwa magwiji wa soka wa kesho. 

"Natarajia kwamba taaluma ya soka nchini Somalia itabadilika sana," anasema. "ITAAL Football Academy itazalisha wachezaji bora ambao wanaweza kushindana, na itahakikisha kwamba kila mtoto wa Kisomali anapata mahali pazuri pa kujifunzia ili kuwa nyota wa soka mtarajiwa.” 

Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.
UNSOM
Awey Haji Nur: Kusaidia vijana Somalia wa leo kuwa mabingwa wa kabumbu kesho.

UN na michezo 

Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu umetambua uwezo wa michezo kuwa na nafasi nzuri duniani, ikiwa ni haki ya msingi na chombo chenye nguvu cha kuimarisha uhusiano wa kijamii na kukuza maendeleo endelevu na amani, pamoja na mshikamano na heshima kwa wote. 

Kwa kuzingatia athari zake nzuri, mwaka 2013, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 6 Aprili kama Siku ya Kimataifa ya Michezo kwa Maendeleo na Amani (IDSDP) kila mwaka ili kutambua athari chanya za michezo na mazoezi ya viungo katika jamii na katika maisha ya watu duniani kote. 

"Michezo ina uwezo wa kuoanisha hamasa, nguvu na shauku yetu kwa lengo la pamoja. Na hapo ndipo tumaini linaweza kusitawishwa na uaminifu unaweza kupatikana tena. Ni kwa maslahi yetu ya pamoja kutumia nguvu kubwa ya michezo kusaidia kujenga mustakabali bora na endelevu kwa wote," alisema Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed, katika maadhimisho ya mwaka huu ya IDSDP. 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed
UN Photo - Jean-Marc Ferre
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed