Elimu bora ni nyenzo muhimu ya kujenga usawa duniani
Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kumeanza mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mabunge duniani, IPU ambapo suala kuu linalomulikwa ni elimu.
Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kumeanza mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mabunge duniani, IPU ambapo suala kuu linalomulikwa ni elimu.
Kuwekeza katika mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF si tu kunafanikisha usaidizi wa kibinadamu bali pia ni kuwekeza katika kuboresha kazi za chombo hicho chenye wanachama 193, amesema Katibu Mkuu Antonio Guterres jijini New York, Marekani hii leo wakati akifungua kikao cha ngazi ya juu cha kuchangia mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2006.
Watu zaidi ya milioni 168 kote duniani mwaka 2020 watahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi katika migogoro inayoendelea kwenye nchi Zaidi ya 50 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu mimasuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.
Meja Seynabou Diouf kutoka jeshi la polisi la taifa la Senegal amechaguliwa na kutangazwa kutwaa tuzo ya polisi mwanamke wa Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2019.
Hii leo katika kuadhimisha miaka 19 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia ukatili wa kingono kwenye mizozo, manusura wa ukatili huo wametoa shuhuda dhahiri za yale waliyopitia huku wakitaka hatua thabiti za usaidizi na uwajibishwaji wa waliowatendea makosa.
Ikiwa leo ni siku ya chakula duniani wito ukiwa ni kutokomeza njaa- na kuwa na dunia ambako chakula chenye lishe bora kinapatikana kwa bei nafuu na kwa watu wote na kila mahali, Umoja wa Mataifa unahoji iweje leo hii zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosheleza mahitaji yao.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wamejulishwa ya kwamba pamoja na hatua zozote zinazochukuliwa kukabiliana na vitisho vya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua za makusudi lazima zichukuliwe kuimarisha vyombo vya dola ikiwemo mahakama na jeshi.
Suala la ulinzi wa wakimbizi ni moja ya vipaumbele vya awali kabisa vya Umoja wa Mataifa takriban miongo saba iliyopita hata hivyo, ufurushwaji wa watu bado unazua wasiwasi mkubwa kimataifa. Taarifa kamili na Arnold Kayanda
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC inauhitaji Ujumube wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO lakini inahitaji MONUSCO iliyo haraka kutekeleza wajibu wake, ulio na vifaa, ulio thabiti na ambao una wajibu sahihi, amesema rais wa DRC, Felix Tshisekedi katika hotuba yake ya kwanza kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Leo Alhamisi Septemba 26.
Rais wa mkutano wa 73 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaotamatishwa hii leo, María Fernanda Espinosa ametaja marufuku ya plastiki zinazotumiwa mara moja na kutupwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuwa moja ya mafanikio makubwa ya kipindi chake.