Shule nyingi duniani hazina maji safi na salama ya kunywa- Ripoti
Je shule anayosoma mwanao ina huduma za maji ya kunywa na vyoo? Au je shule uliyosoma iwe ya awali, msingi au sekondari ilikuwa na huduma hizo muhimu za msingi? Ripoti ya kwanza kabisa inayofuatialia huduma hizo inaonyesha hali mbaya na ya kusikitisha. Kuna shule za msingi hazina kabisa vyoo, maji wala huduma za kujisafi.