Simu zatumika kukabiliana na Ebola maeneo hatarishi DRC

17 Agosti 2018

Shirika la afya duniani WHO limezungumzia mbinu inazochukua ili kufikia walengwa wa chanjo na huduma za kinga dhidi ya Ebola watu walio katika maeneo hatarishi kiusalama huko Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

   Tarik Jasarevic msemaji wa WHO mjini Geneva, Uswisi akizungumza na waandishi wa habari hii leoametolea mfano eneo moja lililo nje ya mji wa Mangina ambako hali ya usalama ni mbaya lakini kumeripotiwa maambukizi, na hivyo wiki iliyopita.

 “Kile ambacho timu zetu imefanya imewasiliana kwa njia ya simu na muuguzi  mmoja wa kijiji hicho ambaye alikuja na wasaidizi wake wawili na kupatiwa mafunzo Mangina jinsi ya kufuatilia waliokuwa karibu na wagonjwa, na wanaendelea kuwasiliana naye kwa simu.”

Halikadhalika kueneza ujumbe wa kinga dhidi ya Ebola ambapo msemaji wa WHO amesema hutumia njia zingine…

“Ujumbe kwa njia ya redio, Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO ina eneo kubwa inasikika na tayari wafanyakazi wa UNICEF wanahamasisha kwa ujumbe.”

Pia amesema ahadi sasa takriban watu 500 ndio wamepatiwa chanjo.

  

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter