Tumeomba mazungumzo na UN wasaidie hali Burundi ili kuandaa Tanzania kuwarejesha wakimbizi - Rais Samia
Tanzania ni moja ya nchi za Afrika mashariki ambazo zimekuwa kimbilio la wakimbizi kwa miaka mingi. Rais wa nchi hiyo Samia Suluhu Hassan alipozungumza na Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipokuwa hapa New York, Marekani anasema ni takribani miaka 50 kwa nyakati tofauti nchi yake imekuwa ikipokea wakimbizi na kwa sasa ameomba mazungumzo na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia wakimbizi UNHCR kusaidia katika nchi wanakotoka wakimbizi ili waweze kurejea akitolea mfano Burundi.