Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo ina mchango muhimu katika amani na maendeleo ya Burundi 

Vijana wakicheza katika uwanja ambao ulikamilishwa na Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS nje kidogo ya mji wa Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo.
UNMISS
Vijana wakicheza katika uwanja ambao ulikamilishwa na Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS nje kidogo ya mji wa Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo.

Michezo ina mchango muhimu katika amani na maendeleo ya Burundi 

Amani na Usalama

Wananchi wa Burundi wameshukuru wazo la Umoja wa Mataifa kuchagiza michezo wakidai imekuwa na mchango katika kurejesha amani nchini mwao kwa kuziunganisha pande zilizokuwa zinakinzana katika masuala ya kisiasa na kijamii.  

Kama usemavyo Umoja wa Mataifa, michezo ni chombo muhimu kwa kudumisha amani na maendeleo. Nchini Burundi, nchi iliyokubwa na mzozo wa kisaiasa na kikabila, michezo ilikuja kuwa chombo maridadi cha kuunganisha waliokuwa wametengana. 

Haji Mosi Yusuf ni Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Burundi, FFB anathibitisha hilo, “Eee Kwa hapa Burundi, michezo ilisaidia sana tukitizama kihistoria ninaweza nikachukulia kwa mwaka 1993 wakati tulipoingia katika machafuko ya kikabila hapa nchini Burundi, mnavyojua ni kwamba mitaa mbalimbali ilikosana na wananchi wa mitaa hiyo ambao ni kabila mbalimbali walikosana na wakaachana kabisa baada ya kufanyika mauaji. Ndio maana upande wa Chama cha Soka nchini Burundi, nilikuwa nimeshakuwa mjumbe, na Kamati ya Olimpiki ilibidi tukae pamoja tukafikiri tufanye kitu ganina ndio ikawa chanzo cha kuanza kuandaa michezo inayohusisha mitaa mbalimbali ya jiji la Bujumbura. Yaani kulipatikana mabadiliko mengi na ndio ikawa chanzo cha watu kuweza kurudi katika mitaa hiyona ikawa chanzo cha wenyewe kuweza kurudi katika mitaa hiyo.”  

Bwana Yusuf anasema mbali na michezo kuleta amani katika jamii ya kirundi, michezo ilileta fursa ya maendeleo katika jamii, “Tumefikia kwenye fani moja ambayo tunazungumzia michezo na maendeleo kwa vijana. Michezo tunataka tuichukulie kama inaweza kuwa ni nguzo mojawapo ya maendeleo upande wa jamii. Na kile ambacho tunapanga kuzungumzia, ni kuhusu mfano wachezaji wa soka nchini Burundi au wakimbiaji kuna mengi wamekwisha yatengeneza katika familia zao. Leo tukienda katika mitaa mbalimbali, huko Mulanvya, Kanyosha na kwingine, tunaona maendeleo wachezaji wamekwisha yafanya katika familia zao, wamejenga majumba mazurimazuri. Hawana uwezo mkubwa wa kupata fursa ya kuweza kwenda shule lakini kimaendeleo, kile kidogo wanachopata hasa hawa wanaocheza nje, wameshafanya mambo mengi na kile wanachopata kinaletwa hapa nyumbani na wameshatoa kwa wafanyakazi.”  

Nzeyimana Germaine ni Raia wa Burundi, mkazi wa jiji la Bujumbura, anakubaliana na kwamba michezo ni kichocheo cha maelewano, amani  katika jamii akisema, “unakutana kama chama cha UPRONA, chama cha CNDD ambacho sasa kinaongoza nchi, unakuta kuna mawazo yale ambayo hayawakutaishi kisaisa, lakini unakuta kwenye mpira, hao watu wanasahau zile sababu ambazo zinawatenganisha au zinawasababisha kila mtu awe na mawazo yake au kupingana unakuta sasa mpira au mchezo wa ujumla, unakuja kuwapatanisha wale watu inakuja kuwaunganisha wanakuwa kitu kimoja. Nikikumbuka wakati ambapo Burundi ilipofuzu kushiriki AFCON nchini Misri, tumeona amaajabu sana, tumeona watutsi, wahutu, wote wamekuja pamoja, wote wakishabikia pamoja, wakisahau yale mammbo ambayo yanawatenganisha.”  

Kuhusu maendeleo ya kiuchumi yanayoletwa na michezo, Bi Germaine anasema ameyashuhudia kwa macho yake, “unaona wengi akina Said Ntibazongiza wana nyumba za ghali hapa kwetu Burundi, akina Cedric Hamis, wanakwenda kule nje ya nchi wanasakata gozi kisha wanajenga magorofa hapa nyumbani na unaona kweli maendeleo nchi inasonga mbele kutokana na hiyo michezo. Kweli hajajajisahau kifamilia, na kweli wanakumbuka hata nchi.” 

Katika nyakati za sasa, vijana wamejikita sana katika michezo na ni sekta zinazoonekana kupendwa na watu wengi kutoka rika mbalimbali.