Skip to main content

Vijana ni nguzo muhimu kwenye kulinda amani:Guterres 

Mejja generali Paulo Emanuel Maia Pereira wa Ureno, naibu kamanda wa kikosi cha MINUSCA.
MINUSCA/David Manuya
Mejja generali Paulo Emanuel Maia Pereira wa Ureno, naibu kamanda wa kikosi cha MINUSCA.

Vijana ni nguzo muhimu kwenye kulinda amani:Guterres 

Amani na Usalama

Katika kuelekea siku ya walinda amani dunaini Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mchango wa vijana katika kudumisha amani ni mkubwa na amani haiwezi kupatikana endapo hawatoshirikishwa.

Baadhi ya vijana Sudan Kusini wakipaza sauti zao na kusisitiza umuhimu ushirikishwa katika jamii wakisema wana mchango mkubwa katika kila nyanja ya maisha ikiwemo masuala ya ulinzi wa amani. 

Na hiyo ndio kaulimbiu ya maadhimisho yam waka huu ya siku ya walindamani ambayo kila mwaka huadhimishwa Mei 27.  

Kupitia ujumbe wake kwa ajili ya siku hiyo Katibu mkuu wamesisitiza kwamba “Katika kila nchi ambako walindamani wanafanyakazi, amani inaeweza kupatikana tu   kwa ushiriki wa kikamilifu wa vijana. Dunia inahitaji kuongeza juhudi kushughulikia mahitaji yao, kupaza sauti zao na kuhakikisha wanashirikishwa katika meza ya maamuzi.” 

Katika ujumbe huo pia Guterres amesema walindamani zaidi ya milioni moja wanawake na wanaume ambao wako msitari wa mbele katika maeneo ya mizozo na wengine zaidi ya 4,000 ambao wamepoteza maisha yao wakiwa kazini huduma na kujitolea kwao asilani hawatosahaulika. 

Amewashukuru wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa 85,000 ambao ni raia, polisi na wanajeshi ambao kwa sasa wanahudumu  katika maeneo yaliyo na changamoto kubwa wakifanya kazi ya kuwalinda walio hatarini zaidi na kuyasaidia maeneo hayo kujenga amani. 

Ameongheza kuwa “licha ya vikwazo vilivyochangiwa na janga la corona au COVID-19 na pia kuwaweka katika hatari ya maambukizi wanawake na wanaume hawa wameendelea kutimiza majukumu yao na kusaidia mamlaka kupambana na janga hilo la COVID-19. Natuma salamu za rambirambi kwa familia za walindaamani waliopoteza maisha kutokana na COVID-19.” 

Katibu Mkuu amesema walindamani hawa wanamjukumu kubwa la kuwalinda na kuwasaidia vijana hususan wasichana na vigori kupunguza ukatili na kudumisha amani. 

Mathallani amesema nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wanawasaidia vijana walio hatarini kuingizwa jeshini na makundi ya wapiganaji na kuwapa suluhu mbadala na endelevu badala ya kushiriki machafuko. 

Nchini Sudan Kusiniamesema ujumuishaji wa vijanam katika mchakato wa amani umesaidia kuimarisha uhusiano baina wadau wa kikanda na kitaif, huku katika nchi kama Mali mpango wa Umoja wa Mataifa MINUSMA na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR mpango wa Umoja wa Mataifa MINUSCA imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na wawakilishi wa vijana ili kuongeza idadi ya wapiga kura katika chaguzi zilizofanyika hivi karibuni. 

Kwa mantiki hiyo Guterres amesisitiza kwamba “Moja ya nguvu yetu kubwa ni vijana wetu walindamani na hasa wasichana walindamani ambao wanachangia kila siku kutokomeza ubaguzi wa kijinsia na kuhamasisha wanawake na wasichana kusaka fursa zingine ambazo si za kitamaduni.” 

Katibu Mkuu amehitimisha ujumbe wake kwa kukumbusha kwamba walindamani wa Umoja wa Mataifa wanasaidia kuilinda amani katika maeneo ambayo ni ya hatari sana duniani. 

Leo na kila siku amesema “Tunaenzi kujitolea na ujasiri wa walindamani wetu kwa kuzisaidia jamii kuachana na vita na kuelekea katika mustakabali salama na imara zaidi.”