Wanawake na wasichana na janga la COVID-19

16 Julai 2020

COVID-19 imeongeza ukosefu wa usawa katika kila sehemu ya jamii, na hivyo kuongeza hatari ya makundi yaliyo hatarini, pamoja na wanawake na wasichana. Janga hili linaongeza hatari ya unyanyasaji wa kinjisia (GBV), inarudisha nyuma maendeleo ya kijamii na ya kiuchumi ya wanawake na wasichana na kutishia afya ya uzazi.

 

 

Zifuatazo ni njia sita ambazo mashirika ya kibinadamu yanazitumia katika kushughulikia mahitaji na vipaumbele vya wanawake na wasichana katika mwitikio wao wa kibinadamu wa COVID-19.

Mpango wa kutoa msaada kwa binadamu wa janga la COVID-19 unaweka mkazo madhubuti katika kukidhi mahitaji ya wanawake na wasichana na kuwawezesha katika nyanja zote za programu yake.Hili linaanza na kuelewa mahitaji hayo. Mashirika ya Umoja wa Mataifa  na mashirika  yasiyo ya kiserikali, NGOs kama Kamati ya  International Rescue Committee and CARE wanachukua mwongozo huu, huko Libya, kwa mfano, CARE ilionesha kuwa kwa wanawake kuna uwezekano wa mara 12 kuliko wanaume kupoteza kazi kwa sababu ya janga hili. Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women linashirikiana na Serikali ulimwenguni kote kuhakikisha wanajumuisha mahitaji ya wanawake na uongozi katika kupambana na C0VID-19.

© UNICEF/Bullen Chol
Mkazi huyu wa akiwa eneo la soko la Konyokonyo mjini Juba nchini Sudan Kusini akivalia vizuri barakoa yake kujikinga na virusi vya Corona. UNICEF ilitengeneza barakoa 6,000 na kuzisambaza kwa wanajamii.

Kushughulikia ukosefu wa chakula kwa wanawake na wasichana

Mifumo ya uzalishaji wa chakula inavyodorora na biashara za mipaka kuzidi kuwa changamoto ndivyo janga hili  linazidi kuongeza viwango vya njaa kwa wanawake na wasichana. Wanawake huwa ndio idadi kubwa ya wafanyikazi wa kilimo lakini wachache wa wamiliki wa shamba, na mara nyingi hawawakilishwi katika kufanya maamuzi ya uzalishaji au usambazaji wa chakula na kwa hivyo hawana uwezo wa kununua chakula kizuri chenye afya  kwa familia zao, na wao na watoto wao wanakabiliwa na hatari kubwa ya ukosefu wa usalama wa chakula na utapiamlo.Katika kujibu tatizo hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP na washirika wake wanatoa kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu katika tathmini ya udhabiti wa kaya zao.

WFP/Tatenda Macheka
Mama akiwafundisha wanae katika wilaya ya Shamva nchini Zimbabwe wakati wa mlipuko wa COVID-19.

Kutoka Colombia hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutoka wilaya zilizochukuliwa na Palestina (OPt) kwenda Yemen, WFP, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, na washirika wa NGO ikijumuisha Oxfam, NRC, Rehema Corps na Save the Children wanalenga kaya zinazoongozwa na wanawake na wasichana walio hatarini kwa kuwapatia vocha ya chakula au msaada wa pesa.

WFP/Simon Pierre Diouf
Mwanamke nchini Mali anatunza shamba ya jamii ambayo ni sehemu ya mradi wa kujenga uwezo wa Chakula Duniani.

Kutoa kipato na msaada wa kazi

Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa linakadiria kuwa nafasi za ajira milioni 195 zinaweza kupotea ulimwenguni kote kwa sababu ya janga la corona, nyingi za nafasi hizi zikiwa ni za sekta zilizo na wanawake wengi.Wakati huo huo, kama mkataba wa mapato unavyodidimia, mahitaji ya matumizi ya nyumbani yanaongezeka kwa vile watu wengi wanakaa nyumbani nazo bei za chakula na vitu muhimu inaongezeka.

IOM
Jamii inajitolea kutengeneza barakoa kwa wafanya wa huduma za Afya huko Cox's Bazar Bagladesh

Kuna hitaji kubwa la kuanzisha miradi yenye mapato ambayo inawalenga wanawake. Huko Bangladesh, UN Women inafanya kazi na shirika kubwa la biashara la BRAC na NGO ActionAid ili kusaidia vikundi vya wanawake wakimbizi wa Rohingya na mashine za kushona na mafunzo ili waweze kutengeneza na kuuza barakoa ili kupata kipato.

Kusaidia kutoa mafunzo 

Mnamo Mei mwaka huu, UNESCO ilikadiria kuwa watoto na vijana bilioni 1.54 pamoja na wasichana milioni 111 wanaoishi katika mazingira ya kipato cha chini  walikuwa hawaendi shule kwa sababu ya  COVID-19. Wasichana wana uwezekano mkubwa kuliko wavulana wa kutokurudi kamwe shuleni.Wengi wanapewa kazi kama kusimamia majukumu ya nyumbani au kutunza wanafamilia, pamoja na wagonjwa, wazee au wanajipata  kwenye ndoa za mapema au kazini, pamoja na kazi ngumu ili kukabiliana na hali ya uchumi.

© UNICEF/Helene Sandbu Ryeng
Angures Buba, mwenye umri wa miaka 14 akitafuta masafa ya matangazo ya elimu ya darasa la 8 kwa njia ya redio. Hapa ni kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na masomo anayosubiria kwa hamu ni Sayansi na Kiingereza.

Wasichana wenye ulemavu ambao ni masikini au wanaishi vijijini wako katika hatari kubwa ya kutokuwa shuleni.UNICEF, washirika wake na mitandao ya maelfu ya wahamasishaji wa jamii wanaeneza uelewa juu ya hitaji la wasichana kuendelea na masomo yao.Mashirika mengi yanayofanya kazi kwenye sekta ya elimu wanaimarisha masomo ya mtandaoni na kwa njia yoyote iwezekanavyo.Masomo sasa yanatolewa kwa redio huko Burkina Faso, Ghana, Rwanda na nchi zingine; kwenye televisheni  huko Ethiopia, Libya na kwingineko na kwenye majukwaa ya kujifunza mtandaoni nchini OPt na Syria.

Kuzuia na kujibu dhuluma za kijinsia

Wanawake na wasichana wako katika hatari kubwa ya kunyanyaswa kijinsia, pamoja na unyanyasaji mwingine wa majumbani kwa sababu ya kudorora kwa uchumi na hatua za kukaa nyumbani ili kuzuia kuenea kwa COVID-19.Simu za dharura na kuomba msaada zimeongezeka kati ya asilimia 30 hadi 75 katika maeneo mengine kwa mfano Zimbabwe ilirekodi ongezeko la asilimia 75, Colombia na Mexico zilirekodi ongezeko la asilimia 50.Katika sehemu zingine kama vile Bangladesh na Iraq, simu hazipigwi tena kwa sababu wanawake hawawezi kutumia au kufikia tena simu katika sehemu zilizo wazi, njia za uhamishaji zinaingiliwa, na vituo vya msaada vimefungwa kwa muda mfupi.Sehemu salama kumi na tisa kwa wanawake na wasichana nchini Syria ilibidi zifungwe kwa muda mfupi kutokana na kuzuia kuenea kwa  COVID-19.

13-07-2020_Unicef_Aweil
Grace (si jina lake halisi) akishona shuka ambalo baadaye ataliuza sokoni. Kitambaa cha shuka amenunua kutoka kituo rafiki kwa wanawake mjini Aweil nchini Sudan Kusini.

Mipango ya kupambana na ukatili wa jinsia wa nchi nyingi ni pamoja na shughuli za kuzuia na ufuatilia kwa kujibu masuala  ya unyanyasaji wa kijinsia,GBV. Katika kaskazini mashariki mwa Nigeria, Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) na wadau huenda nyumba kwa nyumba badala ya kukusanya wanawake katika vikundi ili kuongeza uhamasishaji wa huduma za ukatili wa kijinsia, mashirika ya  misaada pia yanazingatia kutochangamana ili waweze kukaa wazi kila inapowezekana. Kwa mfano, nchini Nigeria, IOM inabadilisha sehemu nyingi na kuzifanya ziwe salama kama vile vibanda vya simu vya kibinafsi ambapo wanawake wanaweza kuongea na washauri.

Mashirika ya Umoja wa mataifa kama lile la kuwahudumia watoto UNICEF na  lile la idadi ya watu duniani UNFPA, na mashirika yasio ya kiserikali, NGO zikiwamo Oxfam na CARE zinaunda na kupanua mitandao ya jamii ili kutoa mwamko juu ya hatari zilizopo kwa wanawake na wasichana kubaini kesi za unyanyasaji wa kijinsia  na ukiukwaji mwingine, na kuunga mkono njia za kutafuta suluho au majibu. Huko Myanmar, Wanawake wa UN Women walipeana simu za rununu kwa wafanyikazi wa jamii 60 kutoka Idara ya Ustawi wa Jamii ili kufanya huduma za simu ziwepo kila wakati ilikusaidia wanawake wanaokabiliwa na ukatili wa kijinsia na  matatizo mengine yatokanayo na COVID-19. Huko Uhabeshi, Shirika la Action Against Hunger yaani hatua dhidi ya njaa, linafanya kazi na Mtandao wa Matangazo wa Oromia kuendesha kipindi cha redio cha kila wiki kuhusu hatari za ukatili wa kijinsia.Walakini, programu za kuzuia na kupambana na ukatili wa jinsia ni ngumu kutoa msaaada , kwani zinafadhiliwa na asilimia 8 tu ya mipango ya kidunia iliyofadhiliwa.

Kudumisha shughuli za kuokoa maisha

COVID-19 imefikia na kuonesha kiwango cha juu kabisa cha mahitaji ya kibinadamu ambayo hayajawahi kutangazwa kote ulimwenguni.Ni muhimu kwamba rasilimali hazipotoshwa kutokana na kazi ya kibinadamu inayoendelea, pamoja na programu za afya zenye kulenga wanawake na wasichana.

© UNICEF/Gabreez
Saba, mwenye umri wa miaka 23 ni mfanyakazi wa kujitolea huko Amran nchini Yemen. Anatumia siku nzima kutembelea jamii na kuelimisha kuhusu COVID-19 na pia kuwaelekeza vituo vya afya.

Mashirika ya misaada kama vile UNFPA na wadau wao wanajaribu kuweka na kuzilinda huduma za kuokoa maisha ya wanaougua magonjwa yanayohusiana na afya ya uzazi kote ulimwenguni.Katika kliniki nchini Syria, kwa mfano, idadi ya wagonjwa imepunguzwa na wafanyakazi wanalazimika kuvaa vifaa vya kinga vya kibinafsi katika maeneo fulani ya kliniki.

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud