Wanawake wapatanishi wa amani wako mstari wa mbele wa kuzuia COVID-19 katika makazi ya wakimbizi nchini Uganda
Ni saa tatu asubuhi jua limeshaanza kutoa miale yake katika makazi ya wakimbiziya Bidibidi katika Wilaya ya Yumbe nchini Uganda. Wanawake wamekusanyikakaribu na kisima cha maji ili kuchota maji ya asubuhi halafu watarudi tena papa hapa jioni.