Kwa pamoja tutalishinda janga la COVID-19:Guterres
Tunakabiliana na tatizo lisilo na mithili yake. Ili kulishinda, ni sharti tuungane.
Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe maalum alioutuma kwenye tamasha maalum la kimataifa la muziki liitwalo “One World Together at Home” au Dunia moja , pamoja nyumbani lililofanyika leo Jumamosi likijumuisha wanamuzikia mbalimbali, wahisani na wadau mbalimbali na wasanii.
Guterres amesema “Leo, kupitia muziki, ambao ni lugha ya wote, tunapongeza ujasiri na kujitolea kwa mashujaa wa afya na wengineo. Tunapofanya hivyo, hebu na tuwakumbuke walio hatarini zaidi.”
Ukurasa kuhusu virusivyacorona & taarifa mpya
Wasomaji wanaweza kupata taarifa na muongozo kuhusu mlipuko wa virusi vya corona (2019-nCoV) kutoka Umoja wa Mataifa, Shirika la afya duniani na mashirika mengine ya UN hapa. Kwa habari mpya kila siku kutoka UN News, bofya hapa.
Amemtaka kila mmoja kujiunga kwenye wito wa usitishwaji mapigano kote duniani ili kujikita na adui yetu sote ambaye ni Virusi.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amewashukuru wote kwa kuunga mkono kazi ya kuokoa maisha ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO na mashirika mengine ya kibinadamu.
Amesisitiza kwamba “Pamoja, tutavishinda virusi hivi na kuujenga ulimwengu wenye usawa zaidi kama raia wa ulimwengu walioungana na mataifa yaliyoungana.”
Penye nia pana njia
Naye Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza kuhusu tamasha hilo amesema penye nia pana njia na kwa pamoja hakuna linaloshindikana , akimuhimiza kila mtu, serikali, wahisani na wadau wote kushikamana ili kukabiliana na adui huyu wa kimataifa COVID-19.