Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN News/Elizabeth Scaffidi

COVID-19 imelazimu kubadili mfumo wa kazi za uandishi wa Habari

 Janga la mlipuko wa virusi vya corona au COVID-19 limelazimisha tasnia ya Habari kufanyia mabadiliko utendaji wake ili kwenda sanjari na hali halisi hasa ukizingatia hivi sasa , shirika la afya duniani WHO linasisitiza hali ya kutochangamana ili kuepusha maambukizi zaidi. Je Afrika Mashariki vyombo na waandishi wa Habari wanaendeshaje kazi zao ili kuhakikisha jamii inaendelea kuhabarika wakati huu wa COVID-19? Hilo ndilo tunaloliangazia leo katika mada kwa kina. Ungana na Flora Nducha

 

 

Sauti
7'38"
Mtoto wa Miaka Saba Francesca(sio jina sahihi)akipata matibabu kutoka kwa Daktari Antonella Tonchiaro ktika makazi yasio rasmi anapo ishi Rome nchini Italy.Daktari Tochiaro ni mmoja wa wafanyikazi wa INTERSOS/UNICEF.
© UNICEF/Alessio Romenzi

Miongozo mipya yatolewa kuhusu njia ya ufunguzi salama wa shule hali itakapotengamaa

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na Benki ya dunia, hii leo mjini New York Marekani, Paris Ufaransa na Roma Italia, wametoa miongozo kuhusu namna salama ya kuzifungua shule kutokana na kufungwa ambako kunawaathiri takribani wanafunzi bilioni 1.3 kote duniani.

Katibu Mkuu Antonio Guterres akitoa ujumbe kuhusu Janga la COVID-19.
UN Photo/Eskinder Debebe)

Usitishaji uhasama kimataifa, kusaidia wasiojiweza na mikakati ya kujikwamua ndio kipaumbele cha UN:Guterres

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo Alhamisi ameweka bayana dhimira ya Umoja wa Mataifa ya kutaka kuvishinda vita dhidi ya janga la virusi vya corona au COVID-19  kwa kujikita na mambo matatu muhimu ambayo ni kufikia usitishwaji wa uhasama kimataifa, kuwasaidia wale wasiojiweza na kujiandaa kujikwamua kiuchumi na kijamii kutoka kwenye janga hili.

World Bank/Maria Fleischmann

COVID-19 yazidisha changamoto za chakula Uganda

 Njanga la virusi vya corona au COVID-19 limewaacha raia wengi nchini Uganda wakiwa na changamoto ya kipato  hali ambayo

imechangia kuongeza changamoto ya uhakika wa chakula.  Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego  mevinjari katika maeneo

mbalimbali kuangazia changamotot za upatikanaji wa achakula na lishe wakati huu ambapo mamilioni ya wanannchi wa kipato

cha chini wanakabiliwa na hatua za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kwa kutokwenda kazini, kufanya biashara   na hata

Sauti
4'3"