Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

‘Uharaka wa kuchukua hatua’ kwa ajili ya maendeleo endelevu, ni mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote wakati janga la corona likiendelea

Umoja wa Mataifa Bangladesh unatoa kipaumbele kwa huduma zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ambazo zimeathirika zaidi na COVID-19
UNDP Bangladesh/Fahad Kaizer
Umoja wa Mataifa Bangladesh unatoa kipaumbele kwa huduma zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ambazo zimeathirika zaidi na COVID-19

‘Uharaka wa kuchukua hatua’ kwa ajili ya maendeleo endelevu, ni mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote wakati janga la corona likiendelea

Ukuaji wa Kiuchumi

COVID-19 ikiendelea inaendelea kuvuruga maisha na ustawi kote duniani, hii leo Jumatatu Umoja wa Mataifa umefanya mjadala mpana wa kisera kusisitiza suluhisho la ushirikiano wa kimataifa ili kupunguza janga wakati pia ulimwengu ukirejea katika mkondo wa kufikia Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu, SDGs.  

Rais wa Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, Mona Juul, amesema “ahadi yetu ya kufikia SDGs haijabadilika, lakini uharaka wa kuchukua hatua umebadilika.”  

Ameendelea kueleza kuwa wakati wa kufanya kazi kuelekea mafanikio ambayo yatasaidia ulimwengu kuondokana na dharura ya dunia, ikiwemo chanjo, “tunaanza kugundua kiwango halisi cha janga la kijamii na kiuchumi ambalo liko mbele yetu.”

Takribani nusu ya nguvu kazi ya dunia iko katika hatari ya kutoajiriwa wakati malengo mengine ya dunia yakirejea nyuma kama vile kuongezeka kwa umaskini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998, kanda nyingine zimerejea katika viwango vya chini vilivyoshuhudiwa miaka 30 iliyopita. 

Viwango vya vifo vitokanavyo na Malaria vinatishia kurejea katika viwango kama vile vya miaka 20 iliyopita na unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana “imekuwa janga kivuli, na idadi ya waathirika ikiongezeka hadi mamilioni duniani kote.” Ameeleza. 

Rais wa ECOSOC amesisitiza kuwa sasa ni wakati wa kuimarisha ushirikiano na mshikamano wa kimataifa.