Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UNICEF/Rebecca Vassie

Guterres:Tukihakikisha haki za wenye ulemavu, tunawekeza katika mustakbali wa Pamoja

Katika mazingira ya kawaida watu wenye ulemavu mara nyingi hukosa fursa ya huduma za msingi kama vile elimu, huduma za afya na fursa za kiuchumi au ushiriki katika jamii.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika uzinduzi wa sera kuhusu watu wenye ulemavu na janga la corona au COVID-19.

Katika uzinduzi huo Bwana Guteres amesema janga la COVID 19 linaathiri kila nyanja ya jamii zetu na leo hii anaelezea jinsi gani janga hili linavyoathiri watu bilioni moja wenye ulemavu duniani.

Sauti
1'25"

06 Mei 2020

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa  tunaangazia habari tofauti kutoka sehemu mbalimbali duniani:

-Tutasikia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu uzinduzi wa sere za  watu wenye ulemavu na janga la corona au COVID-19.

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na jamii ili kusaidia kuepusha kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 hususan kwenye maeneo ya makazi duni huko Kenya.

Sauti
11'18"
UNFPA

Chama cha wakunga Tanzania tunawashauri wakunga wote kutumia vifaa vilivyotakaswa wakati huu wa COVID-19:Lucy Mabada

 Dunia ikielekea kuadhimisha siku ya wakunga hapo kesho tarehe 5 Mei, Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) kimewapa ushauri wakunga wote kuzingatia kuvaa vifaa muhimu vilivyotakaswa hususani wakati huu wa COVID-19 ili kuwalinda watoto dhidi ya maambukizi. Mwaka huu wa 2020 umetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa mwaka wa wa wauguzi na wakunga ili kutambua mchango mkubwa wa wahudumu hawa wa sekta ya afya.

Sauti
3'30"