Neno La Wiki

Neno la wiki- Methali, "mtoto wa nyoka ni nyoka"

Katika Neno la wiki hii Mchambuzi wetu ni mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora ameangazia methali isemayo "Mtoto wa nyoka ni nyoka."

Sauti -
43"

Neno la Wiki- Methali Kandamizi kwa wanawake

Hii leo katika NENO LA WIKI, Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo  anatufafanulia methali za Kiswahili ambazo kwa mtazamo wake zinamkandamiza mwanamke katika jamii. 

Sauti -
6'25"

Neno la Wiki: Mtaka unda haneni

Katika Neno la wiki hii Mchambuzi wetu ni mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora ameangazia methali isemayo "mtaka unda haneni".

Sauti -
45"

Neno la Wiki: Dau, Wadau, Washikadau

Leo katika Neno la Wiki tunabisha hodi Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA ambako mchambuzi wetu,  Bi. Mwanahija Ali Juma, ambaye ni Katibu mtendaji wa baraza hilo anafafanua maneno  “Dau, Wadau na Washikadau" ambayo huleta utata mkubwa katika matumizi yake.

 

Sauti -
1'18"

NENO LA WIKI-“Afugaye ng’ombe tume, mwenye maziwa la kujaza”

eo katika NENO LA WIKI Aida Mutenyo, Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anatufafanulia methali ya Kiswahili isemayo “Afugaye ng’ombe tume, mwenye maziwa la kujaza”

Sauti -
40"

Neno la Wiki- OPOA

Wiki hii katika Neno la Wiki, mchambuzi wetu kutoka Baraza la Kiswahili Zanzibar nchini Tanzania , BAKIZA kwa Bi. Mwanahija Ali Juma , Katibu mtendaji wa BAKIZA akichambua maana ya neno  “OPOA”. Anasema kuwa opoa ni lazima kitu kiwe kinatolewa kutoka kwenye maji!

Sauti -
1'5"

Neno la wiki- Mtoto akibebwa hutizama kichogo cha mamae

Neno la wiki hii leo tunaangazia methali, mtoto akibebwa hutizama kichogo cha mamae. Mchambuzi wetu ni mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora ambaye anasema mtoto hufuata tabia za mlezi au mzazi wake.

Sauti -
1'5"

Neno la Wiki- Methali: Akaae karibu na moto huandaliwa mwanzo

Leo katika NENO LA WIKI Aida Mutenyo, Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anatufafanulia methali ya Kiswahili isemayo “Akaaye karibu na moto huandaliwa mwanzo”. Hii ina maana halisi ya inayoonekana na inayofichika! Fuatana naye.

Sauti -
53"

Neno la Wiki- Baniani mbaya kiatu chake dawa

Neno la wiki hii leo tunaangazia methali, baniani mbaya kiatu chake dawa. Mchambuzi wetu ni mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora ambaye anasema penye baya hapakosi wema!

 

Sauti -
19"

Neno la Wiki- Paraganyika

Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa  Baraza la  Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na  anafafanua neno 'Paraganyika'.

Sauti -
54"