Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

UN News Kiswahili

Neno la Wiki - Kwina

Hii leo Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA Onni Sigalla anakuja neno Kwina akilihusisha sana na suala la kung'an'gania uongozi. Lengo  hasa leo ni kukuongezea msamiati hususan katika kushikilia kitu kupita kiasi au katika sentensi, "Viongozi wetu wana kwina ya madaraka."

Sauti
43"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki: RIKISHA

Hii leo katika Neno la Wiki, mchambuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno RIKISHA.  Anasema kwamba watu wanalitumia wakimaanisha kile kitenzi cha kiingereza, "to leak" lakini kwa kiswahili lina maana tofauti. Je ni maana ipi hiyo? fuatana naye.

Sauti
49"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki- Radhi

Hii leo Ijumaa katika Neno la Wiki, Bi. Mwanahija Ali Juma ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana  ya neno, 'Radhi'. Katika maelezo yake kuna maana zaidi ya  moja,  ikiwemo pale linapotumika kwenye sentensi mathalani, 'fulani kamwaga radhi!' Karibu.

 

Sauti
50"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki - Ulaiti

Katika Neno la Wiki hii leo tunamulika neno Ulaiti na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Na katika uchambuzi wake anasema neno hili linamaanisha aina fulani ya kitambaa. Fuatana naye kufahamu zaidi.

Sauti
59"
UN News Kiswahili

Neno la Wiki- "Pepa"

Na leo katika Neno la Wiki mchambuzi wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "PEPA"

 

Sauti
52"