Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno La Wiki

Habari za UN

Jifunze Kiswahili: Kongamano za Idhaa za Kiswahili Duniani

Katika Jifunze Kiswahili Profesa Aldin Mutembei  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Kiswahili cha Mwalimu Nyerere hivi karibuni nilipokutana naye visiwani Zanzibar Tanzania ambako kulifanyika Kongamano za Idhaa za Kiswahili Duniani, alinidokeza kuhusu jitihada wanazozifanya ili kuwashawishi viongozi wa Bara la Afrika hususani wa Afrika Mashariki kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika hotuba zao wanapokuwa katika majukwaa makubwa ya kimataifa mathalani Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. 

Sauti
57"
Habari za UN

Msemo: KUFANYA AJIZI

Katika jifunze Kiswahili hii leo mtaalam wetu  Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKIZA nchini Tanzania, anatufafanulia maana ya msemo "KUFANYA AJIZI", karibu!

Sauti
1'5"
Habari za UN

MSEMO - Sikio halilali njaa

Na leo Katika jifunze Kiswahili tuko Baraza la Kiswahili la ZANZIBAR nchini Tanzania ambapo hii leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anafafanua msemo “sikio halilali njaa.” 

 

Sauti
1'5"
Habari za UN

Msemo: "TABIA NI NGOZI"

Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda visiwani Zanzibar huko Tanzania ambapo Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa, Zanzibar, BAKIZA Dkt. Mwanahija Ali Juma anafafanua msemo TABIA NI NGOZI, karibu!

Sauti
59"