Neno La Wiki

Neno la Wiki- "Mgeni wa Heshima"

Leo mchambuzi wetu ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anafafanua neno ambalo hutumika ndivyo sivyo“ Mgeni wa heshima."

Sauti -
1'1"

Neno la Wiki: Aghalabu

Katika kujifunza Kiswahili, Mchambuzi Onni Sigalla wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania “BAKITA” anachambua maana na matumizi ya neno “AGHALABU” ambapo anaeleza maana mbili za neno hilo.

Sauti -
1'1"

NENO LA WIKI: Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto

Neno la wiki limejikita katika kuichambua methali isema, 'Kijiko cha jikoni, hakiogopi moto'.  Mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA Ken Walibora anasema methali hii kimsingi inaeleza dhana ya kuwa ikiwa mtu ana mazoea fulani au kazoea mazingira fulani

Sauti -
32"

Neno la Wiki-Matumizi ya neno AFADHALI.

Aida Mutenyo, mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki anachambua matumizi ya neno TAFADHALI.  Anasema kuwa nchini Uganda neno hili ni moja ya maneno yanayowasumbua wazungumzaji wa kiswahili kwani wanalichanganya na neno AFADHALI.

Sauti -
1'48"

Neno La Wiki- Asilani

Hii leo katika Neno la wiki, mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa  baraza la  Kiswahili la Taifa nchini Tanzania-BAKITA na  anafafanua matumizi ya neno Asilani.

Sauti -
55"

Neno la Wiki- Mtondoo haufi maji

Hii leo katika Neno la Wiki, mchambuzi wetu ni Ken Walibora mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA anachambua methali isemayo, Mtondoo haufi maji.  Walibora anasema kwamba methali hii inafananisha mtu aliyezoea mfano shida na k

Sauti -
58"

Neno la Wiki: SAINI na SAHIHI

katika Neno letu wiki hii mchambuzi wetu ni  Mwahija Ali Juma ambaye ni katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar , BAKIZA anafafanua maana ya maneno “SAINI” na “SAHIHI.”

Sauti -
1'25"

Methali: Kizuri hakikosi ila

Katika NENO LA WIKI hii leo mchambuzi wetu Ken Walibora, mwanariwaya na mwanachama wa Chama Cha Kiswahili cha Kitaifa nchini Kenya, CHAKITA anachambua methali Kizuri hakikosi ila.

Sauti -
58"

NENO LA WIKI-KUFA na KUFARIKI

Na sasa ni neno la wiki ambapo Bi. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA anachambua maneno KUFA na KUFARIKI. Bi. Mwanahija anasema kwa kawaida kufa linaweza kutumika kwa mnyama au binadamu.

Sauti -
1'

Neno la Wiki: Meza

Katika Neno la Wiki linachambuliwa neno MEZA.

Na mchambuzi wetu kwa leo ni Aidah Mutenyo Mwenyekiti wa idara za kiswahili katika vyuovikuu Afrika Mashariki

Sauti -
1'22"