Magugu tembo sasa yageuka muarobaini wa mazingira 

Magugu tembo sasa yageuka muarobaini wa mazingira 

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia lengo namba 7 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG unataka serikali, kampuni binafsi na asasi zisizo za kiserikali kujitahidi kuhakikisha nishati mbadala na isiyo haribu mazingira inatumika ili kuepusha uchafuzi wa mazingira na ukataji hovyo miti unaochochea kuenea kwa jangwa. Ni kwa kuzingatia hilo nchini Tanzania kampuni ya Mkaa Mweupe ambao ni rafiki kwa mazingira. Je mkaa huo unatengenezwaje? Basi Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, UNIC,  amezungumza na mhusika ambaye anaanza kwa kujitambulisha na kisha kuelezea kwa kina. 

 

Audio Credit
UN News/ Stella Vuzo UNIC Dar
Audio Duration
2'49"
Photo Credit
UN Tanzania