Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu yangu ya Chuo Kikuu nimeihamishia katika ufugaji wa kuku – Veronica Kyalo 

Elimu yangu ya Chuo Kikuu nimeihamishia katika ufugaji wa kuku – Veronica Kyalo 

Pakua

Kama ambavyo lengo namba 8 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, linazungumzia kazi bora na ukuaji wa uchumi, Veronica Kyalo wa nchini Kenya, pamoja na kuwa miaka nane iliyopita tayari alikuwa na elimu ya juu baada ya kupata shahada ya chuo kikuu katika masuala ya uhasibu, hakupata kazi iliyo bora na hivyo hali yake kiuchumi haikuwa nzuri. Baada ya kufikia uamuzi wa kuanzisha biashara ya ufugaji kuku na uuzaji wa vifaranga, sasa maisha yanakwenda vizuri na amewaajiri watu wengine na hivyo kuchangia katika ustawi wa jamii yake. Mwandishi wetu wa Kenya Jason Nyakundi amemhoji mfugaji huyo. 

Audio Credit
UN News/ Jason Nyakundi-stringer
Audio Duration
3'17"
Photo Credit
© World Bank/Arne Hoel