Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mimba za utotoni sio kupenda kwetu – Wasichana Morogoro

Mimba za utotoni sio kupenda kwetu – Wasichana Morogoro

Pakua

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Watoto – UNICEF, ndoa za utotoni ni zile zote zinanofungwa kabla ya wanandoa kufikia umri wa miaka 18, huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Japokuwa sheria zinapinga ndoa hizi, lakini tabia hii mbaya bado inaendelea ulimwenguni kote. Mbaya zaidi kuwa mara nyingi mimba hizo zinakatisha haki ya elimu kwa watoto hao kwani hushindwa kuendelea na masomo kutokana na sera na sheria za nchi zao. 

Kwa miaka kadhaa nchini Tanzania kumekuwa na harakati za wadau wa elimu na haki za binadamu kutaka watoto wanaokumbwa na kadhia hii kupewa nafasi ya pili ya kuendelea na masomo yao kwani ujauzito huu unawakuta katika umri ambao hawana maamuzi ya kutosha ya miili yao. Katika makala ya leo, John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya Morogoro analiangazia suala hilo katika wilaya za mkoa wa Morogoro. 

Audio Credit
UN News/ John Kabambala -Radio washirika
Audio Duration
3'51"
Photo Credit
UNICEF/UN0118457/