Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko mpya wa COVID-19 watishia ndoto za vijana Uganda

Mlipuko mpya wa COVID-19 watishia ndoto za vijana Uganda

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika hivi karibuni ilionya kuwa awamu ya pili ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 barani humo itakuwa shubiri siyo tu kijamii bali kiuchumi. Nchini Uganda hali hiyo sasa ni dhahiri kwa kuwa takwimu za afya nchini humu zinaonesha  ongezeko la mambukizi kutoka watu 200 mwezi Februari mwaka huu hadi wagonjwa zaidi ya 1,000 kwa siku mwezi Mei na kuilazimu serikali kutangaza maagizo mapya ya kuudhibiti. Maagizo yaliotangazwa mwanzoni mwa mwezi huu ni pamoja na kufungwa kwa tasisi zote za elimu, masoko na usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine.

Hatua hiyo imekuwa na mkwamo kwa vijana hasa wale wanaojipatia kipato kwa kusafirisha bidhaa na abiria kwa njia ya pikipiki au bodaboda. Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego amezungumza na vijana hao kufahamu vile ambavyo wameathiriwa na COVID-19 hivi sasa.

Audio Credit
Leah Mushi/John Kibego
Audio Duration
3'54"
Photo Credit
UN/ John Kibego