Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ndugu watatu wa kiume wajikimu kwa kazi ya ufundi nchini Uganda

Ndugu watatu wa kiume wajikimu kwa kazi ya ufundi nchini Uganda

Pakua

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa zaidi ya asilimia 61 ya watu walioajiriwa duniani, wanapata kipato chao kupitia ajira katika sekta isiyo rasmi. Kwa bara la Afrika, asilimia 85.8 ya ajira zote ni katika sekta hiyo isiyo rasmi ambapo Umoja wa Mataifa unasema idadi kubwa ya waajiriwa huko ni wanaume.

Vijana wengi wahitimu wa vyuo na Vyuo Vikuu hivi sasa wanakwama kupata ajira rasmi na hivyo sekta isiyo rasmi kuwa ndio kimbilio kwa lengo la kufuta umaskini.
Miongoni mwa vijana hao ni ndugu watatu wa kiume nchini Uganda ambao licha ya kutosoma hadi taasisi za elimu ya juu, wameibuka wajuzi wa ufundi kupitia mafunzo waliyoyaona kwa baba yao mzazi na wanatumia kila njia hata mtandao wa intaneti kupata stadi za kisasa za kutengeneza radio na televisheni. Kwa undani kuhusu vijana hawa, ungana na John Kibego mwandishi wetu kutoka Uganda katika makala ifuatayo.
 

Audio Credit
FLORA NDUCHA/JOHN KIBEGO
Audio Duration
3'55"
Photo Credit
UN/ Jason Nyakundi