Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Programu ya 'Dunia yangu bora' imeonesha mafanikio makubwa kwa wasichana Tanzania

Programu ya 'Dunia yangu bora' imeonesha mafanikio makubwa kwa wasichana Tanzania

Pakua

Umoja wa Mataifa ukiwa unapigia chepuo elimu, na kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma, na hivyo kuzisihi serikali na wadau wengine kushiriki katika kutimiza hayo kama sehemu ya kuelekea katika kilele cha Agenda 2030, ulimwengu umeitikia kwa namna chanya ingawa bado jitihada zaidi zinahitajika. Nchini Tanzania, wadau mbalimbali ikiwemo serikali, katika kushiriki juhudi hizo, wamepongeza harakati za Shirika la kuinua wanawake kielimu Tanzania CAMFED, ambalo limekamilisha programu ya ‘Dunia Yangu Bora’ kuwajengea uwezo wa stadi za maisha wanafunzi wa kike mashuleni na waliomaliza kidato cha nne. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time Fm amezungumza na wadau wa mradi huo na kutuandalia makala ifuatayo. Kwanza ni Mratibu wa kitaifa wa mtandao wa Elimu Tanzania Ochola Wayoga. 

Audio Credit
Assumpta Massoi/Hamad Rashid
Sauti
3'9"
Photo Credit
UN SDGs