Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matunda ni lishe muhimu katika mlo wa kila siku

Matunda ni lishe muhimu katika mlo wa kila siku

Pakua

Emmanuel Mwanjisi ni Afisa lishe kutoka hospitali ya Consolatha, Ikonda, katika wilaya ya Makete, nyada za juu kusini mwa Tanzania, akieleza faida za ulaji wa mbogamboga na matunda katika mwili wa binadamu ameeleza kuwa wataalamu wa lishe wanapohamasisha ulaji wa matunda hawamaanishi kuwa ni lazima mlaji ale kiasi kikubwa cha matunda hayo bali kiasi chochote hata kipande kidogo lakini mara kwa mara, kinasaidia kuleta faida mwilini. 

Mtaalamu huyo anaungana na Umoja wa Mataifa katika mwaka huu wa 2021 uliopitishwa kuwa mwaka wa mbogamboga na matunda ili kuhamasisha watu kuzingatia ulaji wa mbogamboga na matunda kwa ajili ya afya zao n ahata kuwa chanzo cha kipato. Kupitia mazungumzo haya na Zawadi Kikoti wa redio washirika Green FM ya Makete, Mkoani Njombe Tanzania, mtaalamu huyo anafafanua zaidi na leo katika sehemu ya pili na ya mwisho anamulika umuhimu wa matunda. 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
3'50"
Photo Credit
Photo FAO/Marco Salustro