Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati mwingine watu wanafanyiwa vitendo vya ukatili lakini hawajui kuwa huo ni ukatili- Mary Nsia Mangu 

Wakati mwingine watu wanafanyiwa vitendo vya ukatili lakini hawajui kuwa huo ni ukatili- Mary Nsia Mangu 

Pakua

Msichana Mary Nsia Mangu wa Arusha Tanzania, ili kuunga mkono Malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs, anaendesha taasisi maalum ya Dexterous Tanzania ambayo ina lengo la kuboresha elimu ya watoto, kuwapatia uelewa kupitia vitabu na pia kuwafahamisha kuhusu ukatili wa kijinsia.  

Vile vile taasisi yake inasaidia kupinga ukatili dhidi ya watoto hususani wa Kike kwa kuwapa elimu kupitia njia mbalimbali ikiwamo kuwafikia moja kwa moja shuleni. Mary anawahamasisha wasichana kuwa majasiri kuleta mabadiliko ndani ya Jamii. 

 

Audio Credit
Anold Kayanda/Mary Nsia Mangu 
Audio Duration
2'53"
Photo Credit
UNMISS\Nektarios Markogiannis