Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanahabari wahaha kutetea mazingira licha ya changamoto

Wanahabari wahaha kutetea mazingira licha ya changamoto

Pakua

Uhifadhi wa mazingira ni miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ikiwa ni nguzo ya kudhibiti madhara ya mabadiliko ya tabianchi ambalo linachagiza mataifa kutunza na kukuza utunzaji wa mazingira.

Lakini kutokana na ukweli kwamba mazingira yanahifadhi rasilimali zinazotakiwa kutekeleza maendeleo, vuta nikuvute imeshuhudiwa kwenye nchi nyingi juu ya rasilimali za misitu na mali nyingine katika maeneo nyeti ikmazingira.

Nchini Uganda hali hii imevuruga uhusiano kati ya wanahabari na vyombo vya dola kama jeshi na polisi na vilevile kampuni binafsi. Wanahabari 7 walikamatwa wakati wakiwa kwenye harakati za kusaka habari kuhusu msitu wa Bungoma ambao eneo liliuzwa kwa kilimo cha miwa. Wanahabari hao waliachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawana hatia yoyote. Sasa Mwandishi wetu John Kibego amezungumuza na Venex Watebawa, Mratibu wa shirika la wanahabari wa mazirigira la WEMNET kuhusu hatma ya kazi ya wanahabari.

 

Audio Credit
Anold Kayanda/ John Kibego
Audio Duration
2'54"
Photo Credit
UN News/ John Kibego