Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taka za mferejini Haiti zageuzwa kazi za sanaa na kuibua vipaji vya vijana waliokata tamaa.

Taka za mferejini Haiti zageuzwa kazi za sanaa na kuibua vipaji vya vijana waliokata tamaa.

Pakua

Kitongoji cha Cité Soleil, kwenye mji mkuu wa Haiti, Port au Prince, unatambulika kwa maisha duni, umaskini uliokithiri na ghasia za kila uchao. Vijana wamekata tamaa! Lakini Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kazi duniani, ILO limeona hali hiyo haiendani sawa na ajenda yake ya 2030 ya kutomwacha yeyote nyuma. Hivyo ilianzisha mradi wa kuibua vipaji vya vijana kupitia kazi za kusafisha mfereji uliokuwa umejaa taka na kuchafua mazingira ya mji huo. Je nini kimefanyika? Na vijana wananufaika vipi hadi kuona tena nuru katika maisha yao? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii. 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Asumpta Massoi
Audio Duration
3'42"
Photo Credit
ILO/Video Capture